• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Ukerewe District Council
Ukerewe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
        • Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
        • Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Maji
    • Uvuvi
    • Kilimo na Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Ongoing Projects
    • Miradi Iliyo kamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Sheria Ndogondogo za Halmashauri
    • Fomu za Maombi
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa kwa Umma
    • Video

JAFO AIPONGEZA UKEREWE KWA UFANISI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: July 30th, 2017

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) amefanya ziara Wilayani Ukerewe kwa dhumuni la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo ametembelea Hospitali ya Wilaya, vituo viwili vya afya ambavyo ni Nakatunguru na Muriti, mradi wa maji Lutare Chabilungo na miradi ya P4R ya mabweni, madarasa na vyoo katika shule za sekondari za Pius Msekwa na Bukongo na kishakuzungumza na watumishi wa halmashauri katika ukumbi mkubwa mikutano.

Naomba nishukuru sana Miradi mingi sana imefanya vizuri hongereni kwa kazi nzuri, nimetembelea mradi wa maji vijijini Lutare Chabilungo kazi imeenda vizuri na ninaamini tukisimamia mradi ule ipasavyo katika sehemu iliyobakia wilaya itakua na uwezo wa kupata maji vijijini kwa wastani wa 77% kutoka 55% hivyo usimamiwe vzuri mpaka mwisho. Alisema Jafo. Mradi unatekelezwa kwa bajeti ya Bilioni 7 ambapo mpaka sasa serikali imeshalipa Bilioni 5.

Ametoa rai marekebisho yafanyike mapema na kama kuna mabomba yaliyo chini ya kiwango yasitumike ilikuiepushia Halmashauri gharama za kununua mabomba pindi mradi utakapo anza kazi. Amemuagiza injinia wa maji wilaya William Kahurananga kuhakikisha vijiji 13 vilivyo kwenye mradi vinapata maji.

Sekta ya afya imekua na changamoto ya upungufu wa dawa hivyo amemwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Revocatus Cleophas kuhakikisha wananunua dawa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi “Pesa zote za kununua dawa zitumike kununua dawa na sio vinginevyo” alisema Jafo. Katika hatua nyingine amefurahishwa na matumizi ya mfumo wa malipo hospitali ukiwa unafanya kazi katika hospitali ya wilaya.

Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri akizungumza nao amewataka watumishi wabadilike katika utendaji wa kazi maana “a business as usual” imekufa na amesema pamejengeka tabia ya watumishi kufanya kazi pekee zenye maslahi. Amewahimiza kuwepo na kipimo cha watumishi katika utendaji wa kazi na kuacha ubabaishaji. Hivyo tubadilike katika utendaji wetu wa kazi na tunaagana ni kwa uweledi gani tunatakiwa kufanya kazi.

Aidha Kupimana kazini kwa mfumo wa OPRAS system imekua haifanyiki ipasavyo katka maeneo mengi imekua ni ya (copy and paste) kama celebration form ya  harusi au zinafanyika pale wakaguzi au upandaji wa madaraja lakini katika sekta binafsi unafanya kazi na utendaji unapimwa hivyo watumishi wa serikali wanapaswa kubadilika na kuanza kuweka mpango kazi wa nini anatarajia kutekeleza lengo moja baada ya lingine na mkuu wa idara afanye hivyo na ikifika mwaka mwingine wa fedha uhakiki ufanyike kubaini malengo mliokubaliana yamefanyiwa kazi au la.

Wakuu wa idara wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo nafasi zao zijazwe na wengine kwani Halmashauri ina wataalamu wengi wazuri wenye elimu kuanzia shahada ya kwanza (Degree) na shahada ya uzamili (masters degree). “Lazima tubadilike”alisema Jafo.

Jafo alisisitiza kuwa tunapeana maelekezo ili tujirekebishe “ukitaka kuruka agana na nyonga”

Katika miradi ya elimu jafo alitembelea shule mbili za sekondari za pius msekwa na bukongo ambazo zililetewa fedha zaidi ya shilingi 500milioni kutekeleza ujenzi wa mabweni ya kulala wanafunzi mawili kwa kila shule, madarasa mannne kila shule na matundu ya vyoo.

 Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Frank S. Bahati kwani miradi mingi imetekelezwa katika ubora unaotakiwa na amewataka kurekebisha baadhi ya changamoto ilikuiletea ukerewe maendeleo

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 20, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA UKEREWE July 23, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WAKUSANYA MAPATO July 27, 2022
  • TAARIFA YA UTOAJI WA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU ROBO YA NNE August 03, 2022
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Mwenge wa Uhuru wakabidhiwa salama wakabidhiwa salama wilaya ya ILemela .

    July 16, 2023
  • Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Col. Deniss F. Mwila atia saini Mkataba wa utekelezaji wa Afua za Lishe utakaotekelezwa wilaya ya Ukerewe.

    October 28, 2022
  • MAKUBALIANO YA UJENZI WA KIWANDA KIDOGO CHA BARAFU WILAYA YA UKEREWE

    October 09, 2022
  • UZINDUZI WA VITABU VYA MAELEKEZO YA JINSI YA KUBORESHA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI WILAYA YA UKEREWE.

    September 08, 2022
  • Angalia Zaidi

Video

FURSA ZA UWEKEZAJI UKEREWE
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • https://www.moe.go.tz/sw/article/tangazo-la-nafasi-za-mafunzo-ya-ualimu-ngazi-ya-astashahada-ya-ualimu-elimu-ya-awali-msingi-na-stashahada-ya-ualimu-elimu-sekondari-sayansi-miaka-mitatu-kwa-mwaka-wa-masomo-20222023
  • Jiwe linalocheza Wilayani Ukerewe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

Tovuti Mashuhuri

  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Necta

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.