Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ni miongoni mwa Halmashauri zilizopokea chanjo za mifugo na heleni za utambuzi wa mifugo kupitia kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo iliyozinduliwa Juni 16,2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Simiyu.
Jumla ya chanjo 217,000 zimepokelewa ambapo chanjo 150,000 ni kwa ajili ya kuku wote ndani ya Ukerewe ili kuwakinga na magonjwa dhidi ya Ndui, Mdondo na Mafua ya kuku.
Awamu ya kwanza ya chanjo hizo tayari imekwisha anza kuanzia tarehe 02 Julai, 2025 ambapo uchanjaji ni kwa ajili ya kuku tu chanjo hiyo inatolewa bure na zoezi linatarajiwa kukamilika ndani ya siku 14.
Aidha chanjo 67,000 ni kwa ya ng'ombe dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu ambayo itakuwa ni awamu ya pili ya zoezi la utoaji wa chanjo hizo sambamba na upachikaji wa heleni 30,000 za utambuzi kwa ng'ombe.
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuwajali wananchi wake kwa kubeba gharama za msingi kwa ajili ya chanjo na utambuzi wa mifugo . Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inatarajia kuchanja jumla ya mifugo 217,000 ambapo kuku ni 150,000 na ng'ombe 67,000.
" Kinga mifugo yako,okoa kipato chako"
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.