Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Wilaya ya Ukerewe wameendesha mafunzo kwa Jumuiya mbili za watumiaji maji lengo likiwa kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya msingi katika utoaji na usimamizi wa huduma ya maji. Jumuiya zilizopatiwa Mafunzo ni Jumuiya za watumiaji maji Mradi wa Maji Bukindo-Kagunguli na Mradi wa Maji Kazilankanda.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe amewapongeza RUWASA kwa kuona umuhimu wa kuendesha mafunzo hayo kwa kamati hizo.
Magembe amewata Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mwanza kuendelea kuangalia kwa Ukaribu Wilaya ya Ukerewe kwani mpaka sasa kuna vijiji ambavyo bado vinahitaji huduma ya maji japo kuwa vipo karibu na vyanzo vya maji.
Aidha amepongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na Mhandisi wa Maji wa Ukerewe kwani pamekuwepo na ongezeko la vijiji vinavyopata maji. Amewataka wanamafunzo kuweka umakini kwa siku zote tatu za mafunzo.
Awali akitoa neno la Utangulizi Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Emmaculatha Raphael ameeleza kuwa mpaka sasa ni vijiji 19 vinapata maji na vijiji 6 vinatarajiwa pia kupata huduma hiyo na Wizara inatarajia kutekeleza Mradi wa Maji wa maeneo yanayozunguka ziwa Victoria na Ukerewe ni vijiji 33 vimewekwa katika mpango wa kupata huduma hiyo.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.