Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ukerewe Bi. Zubeda Kimaro amefungua kikao kazi cha Jumuiya ya Watumia Maji (CBWSOs). Jumuiya za watumia maji zilizoshiriki ni za Mradi wa Maji Kazilankanda wenye thamani ya TSh. 1.7B, Jumuiya ya watumia maji Bukindo- Kagunguli, Mradi wa maji Nansole wenye thamani ya Tsh. 168M na Jumuiya ya watumia maji Muriti-Ihebo wenye thamani ya Tsh. 900M.
Kimaro amawataka kamati hizo kutunza miradi hiyo na vyanzo vyake na kuhakikisha wananchi wanapata maji, pia wametakiwa kutumia nafasi hiyo kutatua changamoto zinazojitokeza. Ametoa Rai ya kuongeza idadi ya watumia maji hata majumbani.
Kaimu Muhandisi wa RUWASA Ukerewe Mhandisi Datius Burchard amewasihi kamati kufanya kazi kwa karibu na kutekeleza majukumu yake na kuboresha yale yaliyo katika uwezo wao kwa kushirikiana na ofisi ya RUWASA.
Burchard amezitaka kamati hizo kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali za Vijiji hivyo ushirikiano uendelee kuwepo.
Aidha Kamati za Jumuiya za watumia maji wametakiwa kushirikiana kwa ukaribu lengo likiwa ni kuhakikisha Miradi ya maji inatekelezwa kwa ubora na kusimamia shughuli Zote ili Mradi hii iwe kwa manufaa ya vizazi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.