Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango inayoongozwa na Mhe. Joshua Manumbu imefanya uhakiki wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika kata za Nkilizya, Kagera, Nakatunguru, Bukanda, Igalla, Kagunguli, Kakukuru, Ilangala na Muriti.
Katika mradi wa Ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Nkilizya walipatiwa Milioni 24, Sekondari ya Buzegwe ilipatiwa Milioni 24 na Sekondari ya Ilangala walipatiwa Milioni 22,156, 569 fedha zote zikiwa ni kutoka mapato ya ndani.
Miradi yote ya ujenzi wa Shule za Sekondari hizo upo katika hatua ya ukamilishaji ambapo kamati imeendelea kuwasihi watendaji kuendelea kuhimiza wananchi kuendelea kuchangia ili kuimarisha miundombinu hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika baada ya kukamilika.
Aidha wajumbe wamepongeza utekelezaji wa miradi hiyo kwani inaenda kuleta tija na kuwaondolea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule.
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango inayoongozwa na Mhe. Joshua Manumbu imepongeza Shule ya Msingi Hamuyebe na Chankamba kwa kutekeleza vema miradi ya P4R.
Wajumbe wamerishishwa na kupongeza Wasimamizi na kamati za ujenzi katika maeneo hayo baada ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kutembelea na kukagua miradi hiyo na kubaini kuwa thamani ya fedha imeonekana.
Shule ya Msingi Hamuyebe ilipokea kiasi cha Tsh 47,700,000 kujenga vyumba viwili na choo cha wanafunzi matundu saba na Shule ya Msingi Chankamba ilipokea kiasi cha Tsh 45,500,000 kujenga vyumba viwili vya madarasa na vyoo vya wanafunzi matundu matano ambapo mpaka sasa miradi yote ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia Mapato ya Ndani imetekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa vyoo katika soko la Monachi na Kakukuru lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira mazuri ya kufanyia biashara.
Mradi wa Ujenzi wa choo matundu mawili na bafu soko la Monachi Kiasi cha Tsh 5,996,500. Kimetumika na Ukarabati wa Choo soko la Kakukuru umegharimu Tsh 779,000 na mpaka sasa mradi umekamilika.
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamepongeza miradi hiyo kwani imelenga kuhudumia wafanyabiasha na kutunza mazingira ya kufanyia kazi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.