Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Leo imefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika kata ya Irugwa iliyopo kisiwani.Miradi iliyotembelewa ni katika sekta ya Elimu na Afya.
Mhe. Gabriel K. Gregory Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji ambaye ni mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ameongoza kukagua miradi hiyo akiwa na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ikiwa na Kaimu Mkurugenzi Bw. Goodluck Mtigandi
Mradi wa Ujenzi wa Bweni la wanafunzi Limegharimu kiasi cha Milioni 80 na mchango wa wananchi 11.9 Mradi huu umekamilika na Mradi unatumika na Bweni Linauwezo wa kubeba wanafunzi takriban 100.
Kamati imewapongeza wananchi kwa kujitoa kwa kuchangia shughuli za Maendeleo kwani wamefanya vizuri na thamani ya Fedha inaonekana.
Kamati imeshauri pia kuweka na vizima moto katika Bweni hilo kwa Usalama zaidi na
Imeelekeza makadirio ya gharama ujenzi katika kisiwa hiki yasiwe sawa na kisiwa kikubwa kulingana na umbali uliopo kati ya kisiwa kikubwa na Irugwa.
Kamati imekagua Zahanati iliyojengwa na wananchi katika kijiji cha Nabweko ambapo mpaka sasa imegharimu kiasi cha Tsh. Milioni 40 na mfuko wa jimbo ilitoa mifuko 100 na mapato ya ndani Milioni 10 na ujenzi unaendelea.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.