Kamati ya Fedha Utawala na Mipango inayoongwazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe. George Machera Nyamaha pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Ester Anania Chaula pamoja na menejimenti. Leo wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa fedha za serikali.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, bweni na ukamilishaji wa boma la chumba kimoja cha darasa katika shule ya sekondari Bukongo kiasi cha Tsh. 127,500,000.00. katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Tsh.40,000,000.00 zilizopokelewa mpaka sasa jumla Tsh. 6,380,000 zimekwisha tumika. Kamati imeshauri ujenzi wa ngazi maalumu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu ufanyike na usimamizi wa karibu ufanyike ili mradi ukamilike kwa wakati. Ujenzi wa bweni moja Tsh. 75,000,000 ujenzi upo hatua ya ukamilishaji wa boma wajumbe wamepongeza na kuridhika katika hatua ya utekelezaji wa mradi huo. Ukamilishaji wa Boma moja la darasa Tsh. 12,500,000 utekelezaji upo hatua nzuri.
Ukamilishaji wa vyumba viwili (2) vya madarasa katika shule ya sekondari Lugongo Tsh. 25,000,000 ambapo mradi upo kwenye hatua ya ukamilishaji na upakaji rangi ukuta unaendelea pamoja na utengenezaji wa meza na viti 80 za kusomea unaendelea.
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na choo chenye matundu 6 shule ya msingi Murutunguru kwa fedha za P4R Tsh. 46,000,000. Ujenzi upo hatua ya ukamilishaji ambapo mpaka sasa jumla ya Tsh. 33,759,300 zinatumika. Hatahivyo wajumbe walitoa ushauri kuwa ziwekwe ngazi kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu.
Utekelezaji wa mradi a kitalu nyumba (Green house) katika kijiji cha Bugorola Tsh. 16,874,900 ujenzi umekamilika na uwekaji wa mifumo ya mabomba kwa ajili ya umwagiliaji (drip irrigation) umekamilika kwa kiwango cha kuridhisha. Vijana 100 wamepata mafunzo ya kufanya kwa vitendo na uzalishaji wa bustani katika kitalu nyumba hicho. Wajumbe walipongeza mradi huo na kusisitiza vijana wawe walengwa wakuu wa mradi huo.
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na choo chenye matundu 6 katika shule ya msingi kalendeleo Tsh. 46,000,000. Ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji, ujenzi wa boma la choo umekamilika na mpaka sasa jumla ya Tsh. 38,489,000 zimetumika.
Ujenzi wa nyumba 6 za walimu shule ya sekondari Busangumugu kwa fedha kutoka TEA Tsh. 150,000,000. Ujenzi po katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ikiwemo ufungaji wa renta. Wajumbe waliridhika na utekelezaji wa mradi huo, kamati imeelekeza kuwa jitihada na kasi iongezwe ili ikamilike kwa wakati.
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na choo chenye matundu 6 shule ya msingi Kakerege kw fedha za P4R. mpaka sasa ujenzi upo kwenye hatua ya ukamilishaji ambapo madarasa yameezekwa na kupigwa lipu na kwa upande wa choo upigaji wa lipu unaendelea. Wajumbe wameridhika na hatua za utekelezaji wa ujenzi huo.
Wataalamu wameahidi kuendelea kutekeleza miradi yote kwa ufanisi zaidi na kukamilika kwa wakati ili kuweza kuwahudumia wahusika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.