Kamati ya Utawala fedha na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. George M. Nyamaha pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo imetembelea Bandari ya Bukimwi kata ya Ngoma na kuona shughuli ya usafiri inayofanywa na Kivuko cha Mv. Ilemela inayofanya safari yake kati ya Kayenze-Bezi-Ukerewe.
Kamati imepongeza hatua ya Serikali kuanzisha safari hizo kwani wengi watanufaika.
Kamati ya Utawala fedha na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. George M. Nyamaha pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo imefanya ikaguzi wa Miradi ambapo imetembelea utekelezaji huo katika Uezekaji wa jengo la utawala shule ya sekondari Mumbuga unaogharimu 4,000,000/-, Uezekaji wa jengo la Nyumba ya mwalimu Shule ya msingi Nantare Tsh 25,000,000/-, madarasa Vyumba 3 shule ya msingi Murusuli Tsh 9,100,000/-, kuezeka zahanati Musozi Tsh 10,000,000/-, ukamilishaji wa chumba cha darasa la awali Na Choo cha wanafunzi shule ya msingi Musozi Tsh 15,000,000/- Fedha zilizotolewa Na TAHEA, kuwezesha ukamilishaji wa Nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kagunguli 2,840,000/-. Miradi yote ikokatika hatua ya ukamilishaji ambapo Kamati imeelekeza miradi hiyo kukamilika kwa wakati.
Aidha Kamati ya Utawala, Fedha Na Mipango imetembelea kukagua Ujenzi wa Chuo cha VETA kilichopo kijiji cha Muhula Mradi unagharimu takribani bilioni moja Na mpaka sasa Ujenzi umeanza Na upo katika hatua ya kujenga Msingi. Kamati imeishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujenga chuo hiko Na kuahidi kwa changamoto yoyote watakayokutana nayo wajulishwe Na waweze kutatua ili Mradi ukamilike kwa wakati ili watu waanza kunufaika.
Siku ya pili Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango pamoja na wakuu wa Idara na vitengo wameendelea na ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo wakiongozwa na Mhe.Gabriel gregory Kalala Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na kutembelea miradi ambayo ni Uezekaji wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Mandela Tsh 5,000,000/- kutoka mfuko wa jimbo, Uezekaji jengo la maabara shule ya Sekondari Mukituntu Tsh 2,000,000/- fedha zilizotolewa na nfuko wa jimbo.
Ukamilishaji wa chumba cha darasa la awali na choo Shule ya Msingi Nsenga Tsh 15,000,000/- zilizotolewa na TAHEA. Ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kitanga serikali kuu ilitoa Tsh 25,000,000/-, Ukamilishaji darasa la awali na choo shule ya msingi Isisi Tsh 15,000,000/- kutoka TAHEA, Uezekaji maabara Sekondari ya Busangumugu Tsh 3,000,000/- kutoka Mfuko wa Jimbo.
Kamati imeridhishwa na miradi hiyo na kuwataka watendaji na wakuu wa shule kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kwani mpaka sasa ipo katika hatua ya uezekaji na ukamilishaji.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.