Kamati ya siasa ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi inayongozwana Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe Ally Mambile na wajumbe wake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estomin F. Chang’ah, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Frank Bahati na wakuu wa idara na vitengo wote wametembelea miradi mbali mbali inayotekelezwa wilayani Ukerewe.
Miradi wa Maji Chabilungo unaoendelea kutekelezwa kwa Fedha za Serikali ambapo mpaka sasa unatarajiwa kuwahudumia wananchi wengi, kamati ya siasa imeshauri wataalamu waendelee kutoa elimu na hamasa wananchi kutumia maji hayo kwani na safi na salama. Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya Datus Buchard ameleza kamati kuwa jitihada za kuhamasisha watu kuunganishwa ilikupata maji kwenye ngazi ya kaya zinaendelea.
Mradi wa Daraja lililokuwa limekatika na kujengwa kingo zake upya ni moja ya miradi ambayo kamati ya siasa ya wilaya imetembelea na kupongeza kwani daraja hilo ni moja ya kiunganishi cha maendeleo katika maeneo hayo. Ujenzi wa dara hilo ni kiasi cha shilingi milioni 30 na mpaka sasa ujenzi umekamilika na daraja linafanya kazi. Mwenyekiti wa CCM Ally Mambile na Mkuu wa Wilaya Estomin Chang’ah wamewataka wananchi wa eneo hilo kuzingatia kanuni a kutokulima katika vyanzo vya mito.
Kamati ya siasa ya wilaya imetembelea pia mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Bwisya fedha zilizotolewa na serikali milioni 400. Ujenzi wa kituo cha afya unamajengo sita ambayo ni nyumba ya mtumishi, jingo la maabara, jengo la wazazi, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, na kichomea taka. Majengo haya yapo kwenye hatua mbali mbali kama kupauwa, kuweka mfumo wa maji na umeme. Kwa niaba ya Mhandisi Wilaya Robert Magayane ameeleza kuhusu mradi huo na amebainisha baadhi ya changamoto zikiwemo jiografia ya eneo pamoja na usafirishaji wa vifaa.
Mambile amepongeza hatua zilipofikia katika ujenzi huo na amewataka wataalamu kuendelea hivyo katika hatua za ukamilishaji ili mradi huo uwe wa mfano katika Mkoa wa Mwanza. Nae Frank Bahati ameiambia kamati kwa kushirikiana na wataalamu atahakikisha kituo hiko cha afya kinakamilika na kuanza kuwahudumia wananchi.
Mradi wa Maabara ya fizikia katika shule ya sekondari Pius Msekwa inayondelea kujengwa ambapo mpaka sasa imetumia milioni 18 na bado inaendelea kijengwa na ilikukamilika inahitajika kiasi cha shilingi milioni 18 ilikuanza kutumika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.