Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Mazingira Mhe. Felician Manyonyi Diwani wa kata ya Bukongo ameongoza kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ihusuyo uchumi. Viongozi wengine walioshiriki katika uhakiki wa miradi hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Joshua Manumbu, makamu Mwenyekiti Mhe. Athanas Kiza Marobo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Ester A. Chaula.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa Marekebisho ya Stendi Choo, na Mitaro, eneo la maegesho ya magari na jengo la mlinzi thamani ya Tsh. Milioni 16wajumbe Wameshauri ukamilishaji wa mradi na marekebisho yote yafanyike haraka.
Kikundi cha Vijana kumi walipatiwa mkopo wa Tsh 10 M na walinunua pikipiki 4. Kamati imewashauri kuwa na ofisi za kikundi chao nae Mkurugenzi Mtendaji Bi. Ester A. Chaula amewahimiza kurejesha kwa wakati na wakilipa kwa muda itawapa nafasi ya kuomba mkopo mkubwa zaidi ili wainue na wengine.
Kikundi cha walemavu Sokokuu walipatiwa Tsh. 3M, Kikundi cha wanawake sungura walipewa 5M wanachama 39 wametakiwa kurejesha kwa wakati na itawasaidia kupewa mkopo zaidi pia kupitia marejesho hayo yatawezesha wengine kupata mkopo.
Vizimba vya kupimia samaki vimejengwa kwa Tsh. 2,3M katika mialo lengo likiwa kupima mazao ya samaki na kuongeza mapato ya Halmashauri ushauri marekebisho madogo ya ukamilishaji yafanyike.
Shamba la machungwa la Bw. Ladslaus Mlagala amepanda miche 534 aliyopewa na Halmashauri pamoja na shirika la MVIWAU kwenye eneo la takribani Heka 9 miti alioanza kupanda 2019 mpaka sasa.
Bugorola Green house (shamba darasa) Mradi wa Tsh 16M umejengwa mwaka 2019 kama Shamba la mfano lina vijana 100.
Mradi wa Chama cha Ushirika BUKASIGA waliopo Kata ya Kakukuru Walipewa mkopo na Benki ya Kilimo Tsh 200M ili kutekeleza Mradi wa kutengeneza barafu kwa ajili ya wafanya biashara wa samaki. Uzalishaji wa barafu kwa saa 24 wanapata Tani 5
Kamati imewapongeza kwa kuendesha mtambo wenye tija, Aidha wameshauriwa kuomba mkopo kama kikundi kwa kufuata taratibu. Hatutegemei Mradi unakufa Bali uendelee na kusambaa maeneo mengine ya ukerewe
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.