Kamati ya uratibu wa mbio za mwenge wa uhuru 2025 mkoa wa Mwanza leo Julai 14, 2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa uhuru mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ndugu Alan Augustine Mhina akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ukerewe na timu ya menejimenti ya Halmashauri ndani ya Wilaya hiyo ambaye amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo, huku akisisitiza kuwa Ukerewe ndio itakuwa mwenyeji wa mapokezi ya mbio hizo ki mkoa.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa hoteli ya Halmashauri kwa fedha za mapato ya ndani , vyumba vya maduka ya biashara, barabara katika kata ya Nansio ,mradi wa maji kata ya Muriti pamoja na eneo la mapokezi katika viwanja vya shule ya msingi Muluseni kata ya Ngoma.
Ukaguzi huo ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupita Wilaya ya Ukerewe mnamo mwezi Agosti 2025 ukilenga kuhakikisha miradi yote inayotarajiwa kutembelewa imekamilika kwa viwango vinavyostahili.
Kauli mbiu ya Mwenge kwa mwaka huu 2025 ni:
“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.”
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.