Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat S. Kandege ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa manne na ofisi moja katika Shule ya Msingi Murunsuli.
Kandege amepongeza wananchi wa kata ya Ngoma kwa kuonyesha mshikamano na kujenga vyumba hivyo vya madarasa ikiwa na lengo la kukabiliana na upungufu wa Madarasa.
Mhe Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe ameeleza kuwa kwa kupitia nguvu za wananchi na uhamasishaji aliofanya zaidi ya vyumba vya madarasa 316 vinejengwa na vipo vilivyoanza kuezekwa na Halmashauri na vingine Bado.
Magembe ameomba wizara kuangalia na kuwezesha fedha ilikuweza kuenzeka maboma hayo. Amewapongeza wananchi wa Murunsuli kwa kujenga madara hayo na sasa yapo katika hatua ya kuweka madirisha na ukamilishaji.
“Hakika kuna vingi vya kujifunza kutoka ukerewe hongereni wananchi kwa ujenzi huu na wengine igeni mfano huu”. Alisema Kandege.
Gharama za Ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya waalimu Halmashauri imetoa Tsh 13,054,000/-, michango ya wananchi Tsh 11,000,000/-, nguvu za wananchi 6,000,000/-.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat S. Kandege amekagua shughuli za utendaji kazi wa vikundi vya kijamii ambavyo vimepatiwa mkopo na Halmashauri kupitia vikundi ambapo ni utekelezaji wa Sheria kuwa asilimia 10 ya pato la Halmashauri inatakiwa kukopeshwa wanawake vijana na watu wenye ulemavu.
Kandege ameelekeza Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii kuongeza kiasi cha mkopo na kuwa kiwango cha chini kikundi kukopeshwa kiwe TSH 5,000,000/-.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo Secilia Oswago ameeleza Halmashauri inatekeleza sheria hiyo na vikundi alivyotembelea Naibu waziri vimewezeshwa kikundi cha Tumaini Jema kata ya Kagera kimekopeshwa TSH 5,000,000/- na chama cha watu wenye ualbino kimekopeshwa TSH 2,000,000/- na wote wanatarajiwa kurejesha baada ya mkopo ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine kukopeshwa.
Bi. Ester A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ameeleza kuwa Halmashauri inaendelea kutoa mikopo hiyo na kwa mwaka huu wa fedha Halmashauri imeshatoa jumla ya TSH 103,950,000/- na Bado utoaji wa mikopo mingine utafanyika.
Kandege amepongeza vikundi hivyo kwa ubunifu walionao kwani bidhaa zao ziko katika ubora unaotakiwa.
Aidha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat S. Kandege ametembelea na kukagua majengo na utoaji Huduma katika kituo cha Afya Bwisya kilichopo kata ya Bwisya Tarafa ya Ukara.
Kandege ameridhishwa na Kituo cha Afya hiko ambapo amepongeza Serikali ya Wilaya ya Ukerewe kwa kutekeleza vema ujenzi huo ulio gharimu takribani Bilioni 1.2.
“Ukiita Kituo cha Afya unakua hutendi haki kinastahili kuitwa Hospitali ya Wilaya” alisema Kandege.
Mhe Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe ameeleza mahitaji yote yanayohitajika katika kituo hiko ilikufanya kuwa Hospitali ya Wilaya ikiwemo watumishi na baadhi ya vifaa yamesha wasilishwa Wizarani na nimatumaini kuwa yatafanyiwa kazi.
Kandege ameeleza kuwa Adhma ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt John Magufuli ni kuhakikisha Afya za wats za is zinaimarika hivyo ametangaza kuajiri madaktari 1000 ambapo ajira za madktari 750 zitakua TAMISEMI hivyo ameahidi ataleta madaktari wasiopungua watatu katika kituo hiko.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.