Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike Leo ameanza Ziara ya siku mbili kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya ukerewe ambayo ni ujenzi wa madarsa katika tarafa za ukara na mumlambo lengo likiwa nikukagua Kituo cha Afya Bwisya ambayo itakua na hadhi ya Hospitali ya Wilaya na ujenzi wa madarasa Fedha iliyotolewa na Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko19.
Samike ametembelea Miradi kisiwa cha Ukara na amewataka amewataka wakuu wa Shule na kamati inayosimamia ujenzi kuhakikisha inasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika katika ubora unaotakiwa.
Aidha Amelekeza kuwa Shule za Sekondari Bukiko, Nyamanga na Bwisya kupanda miti katika maeneo yao hii italeta mandhari nzuri ya Shule na utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameelekeza kasi iongezeke katika utekelezaji wa ujenzi wa madarasa na kuhakikisha ubora unazingatiwa na Miradi yote ikamilike kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Bw. Emmanuel Sherembi ameeleza kuwa kwa changamoto za kisiwa cha Ukara nyingi zimetatuliwa na miradi inaendelea vema.
Katika Tarafa ya Ukara ametembelea Shule za Sekondari Bwisya inayojenga madarasa 5, Nyamanga inayojenga madarasa 7, na Bukiko inayojenga madarasa 4 na Tarafa ya Mumlambo ametembelea Shule za Sekondari Bukindo inayojenga madarasa 8, Pius Msekwa inayojenga madarasa 5 na Tarafa ya Mumbuga amekagua Shule ya Sekondari ya Bukongo inayojenga madarasa 3 ambapo kila darasa Serikali ilitoa Tsh. 20,000,000.00.
Katika siku ya pili ya ziara yake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameendelea na ziara ambapo amepata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe na ametembelea Miradi ya Maendeleo katika kisiwa Kikubwa cha Ukerewe.
Samike akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe amewataka waendelee kufuata Sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma. “ kila Mtumishi kwa nafasi yake anawajibu wa kutekeleza mambo yote ya msingi kwa kufuata sheria na miongozo ya utendaji kazi ili kutoa Huduma bora kwa wananchi” Alisema Samike.
Aidha amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuwezesha Halmashauri kujiendesha katika shughuli za kila siku.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Emmanuel Sherembi ameahidi kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanywa kwa uaminifu na kuziba mianya ya upotevu wa mapato.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza amekagua Ujenzi wa Madarasa katika Shule za Sekondari Nakatunguru waliopatiwa Tsh. 60,000,000.00 kujenga madarasa matatu na sasa wapo hatua ya kupandisha kuta usawa wa madirisha, Shule ya Sekondari Bukanda iliyopewa Tsh. 100,000,000.00 kujenga madarasa matano na wapo hatua ya kukamilisha kupiga kenchi na Shule ya Sekondari Mumbuga iliyopewa Tsh. 120,000,000.00 kujenga madarasa 6 na mpaka sasa wapo hatua ya kupandisha kuta.
“Ongezeni kasi ya ujenzi wa madarasa na yakamilike kwa wakati uliopangwa na Serikali” Alisisitiza Samike.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.