Halmashauri ya Wilaya Ukerewe Mkoani Mwanza leo imezindua zoezi la Unyunyiziaji dawa ya Ukoko majumbani, uzinduzi umefanyika katika kata ya Namagondo kijiji cha Namagondo na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Kanali Denis Filangali Mwila akiwa na kamati ya Ulinzi ya Wilaya kwa kushirikiana na shirika la Abt Associates kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la misaada kutoka Marekani.
Kanali Mwila ametoa wito kwa wananchi wote wa Wilaya ya Ukerewe kutoa ushirikiano kwa wanyunyiziaji wanapofika katika Kaya kupuliza dawa hiyo kwani lengo ni kuhakikisha malaria katika Wilaya ya Ukerewe inapungua zaidi kwani kwa takwimu mpaka mwezi Oktoba 2021 Ukerewe tumefanikiwa kupunguza kiwango cha maambikizi ya malaria kufikia 31.2% lengo la taifa ni kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kifikia 3.5 ifikapo mwaka 2025 ambapo hali ya uambukizo itapungua kwa 74%.
Dk. Getera Nyangi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa ipo mikakati ambayo imekua ikitekelezwa katika kupambana na ugonjwa wa malaria ni pamoja na kutoa elimu ya afya juu ya madhara ya ugonjwa wa malaria, kuhimiza na kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kila mwisho wa mwezi, zoezi la unyunyiziaji dawa ya kibiolojia (larviciding) ili kuharibu mazalia ya mbu waenezao malaria na upuliziaji wa dawa ya ukoko majumbani.
Bw. Joshua Mutagahywa Afisa Mazingira na Usalama ABT ameeleza kuwa zoezi hili ni awamu ya tatu kufanyika unyunyiziaji. Zoezi la mwaka limeanza tokea tarehe 18/11/2021 na kumalizika tarehe 18/12/2021 na Kaya zote wilayani zitapuliziwa na wapuliziaji 517 katika vituo au kambi 25 kwa Wilaya nzima.
Bi. Magdalena Joseph Mkazi wa Namagondo amewatoa hofu wananchi wote wa ukerewe wenye mashaka na dawa hiyo na kupelekea kuzuia wapuliziaji kufanya kazi yako kuacha kwani dawa hiyo inamaliza mbu kabisa kwenye nyumba na haina madhara kama wanavyofikiria.
Mwisho.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.