Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel B. Magembe amehitimisha mafunzo ya jeshi la akiba wilayani Ukerewe. Hafla ya kilele cha mafunzo ya jeshi la akiba wilayani ukerewe imefanyika leo katika viwanja vya ukuta mmoja na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, viongozi mbalimbali wa wilaya pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Sgt. Rumanyika Aloyce Rwechungura Ambaye ni Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ukerewe ameeleza kuwa idadi ya walioanza mafunzo walikuwa jumla ya watu 168 wanaume 138 na wanawake 30 na mpaka kufika siku ya kuhitimu mafunzo wamehitimu leo wakiwa 88, wanaume 70 na wanawake 18 wakiwa ndiyo washindi waliofaulu mafunzo ya jeshi la Akiba kutoka katika wilaya ya Ukerewe.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Cornel B. Magembe amewapongeza wahitimu wa mafunzo ya jeshi la Akiba kwa juhudi na nia ya uzalendo walio nayo, na Kuwatia moyo wahitimu wa jeshi la Akiba kutokana na changamoto wanazokutana nazo wakati wa mafunzo ikiwemo jamii kuwacheka na kuwadharau, kukosa sare na kukosa ushirikiano mzuri wa wananchi watakao tumikiwa na jeshi hili.
Magembe amewataka na kuwashauri wananchi wa wilaya ya ukerewe kujiunga na kuona faida ya jeshi la Akiba, na Kuahidi kutoa ushirikiano kuwa wanapata mafunzo ya awamu ya pili baada ya kuhitimu kwa awamu ya kwanza.
Aidha amewashauri wahitimu kuwa wanafaida kubwa ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa hivyo wanahitajika kukizi vigezo kama vile cheti chenye ufaulu mzuri yaani kidato cha nne au cha sita, kuwa na cheti cha kuzaliwa. Na Kuahidi kutekeleza ombi la kununua sare ya jeshi la Akiba pamoja na Kuhakikisha waajili wenye uhitaji wa askari wanaajili mtu au watu waliopitia na kufuzu jeshi la Akiba ili kuhakikisha usalama wa eneo husika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.