Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia divisheni ya afya, ustawi wa jamii na lishe imeungana na Halmashauri nyingine nchini kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani kwa kutoa elimu ya afya inayohusisha mama na mtoto sambamba na huduma nyingine za uzazi na utoaji chanjo kwa watoto katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ndani ya Wilaya ya Ukerewe.
Ditrum Kutumile ni Afisa lishe wa wilaya hiyo, amezungumza na baadhi ya kina mama waliojitokeza kupata huduma mbalimbali za afya kwa watoto wao katika kituo cha afya Nakatunguru kilichopo kata ya Nakatunguru ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
"Kauli mbiu ya mwaka huu inasema thamini unyonyeshaji, weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto inaonyesha namna ambavyo dunia nzima inatambua umuhimu wa mama kuanzia suala zima la unyonyeshaji."
Ditrum amewaasa kina mama kunyonyesha watoto ili kuwajenga vizuri kiakili na kuachana na fikra potofu za kunyonyesha kwa muda mfupi ili kulinda matiti yasianguke.
Nae Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt.Pascal Moshiro amezungumzia sera ya taifa ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili inayotoa katazo la watoto wenye umri chini ya miezi 6 kupewa vyakula mbadala,huku ikiweka wazi watoto kuanza kupewa vyakula vya nyongeza wanapotimiza umri wa miezi 6 na kuendelea.
Akitoa elimu ya namna bora ya kunyonyesha Afisa lishe wa hospitali ya Wilaya ya Ukerewe Bi.Julieth Peter ametoa faida za mama kunyonyesha mtoto ipasavyo ikiwa ni pamoja na mtoto kupata afya nzuri kwa sababu maziwa ya mama yana viinilishe vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.
Faida nyingine ni kuleta upendo baina ya mama na mtoto,inapunguza hatari ya mama kupata saratani ya matiti,inatumika kama njia ya uzazi wa mpango endapo mama atanyonyesha ipasavyo na pia maziwa ya mama hayana gharama yapo tayari muda wote kinachohitajika ni usafi wa mwili wakati wote.
Jesca Masinde ni miongoni mwa kina mama waliopata elimu ya unyonyeshaji yeye ni mkazi wa mtaa wa Miti mirefu uliopo kata ya Nakatunguru anasema amenufaika na elimu hiyo kwani kuna vitu kama kumpa maji mtoto mchanga alikuwa anaona sawa.
Maadhimisho ya wiki ya unyo
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.