Kongamano la kidini la Maadili, Amani na Uzalendo lafunguliwa na mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe SP. Osward Bankobeza. Kongamano hilo lilihudhuliwa na Kamati ya MKoa ya Amani ikiongozwa na wachungaji, Mapadri na Mashehe. Wakiambatana na wajumbe wa Kamati ya Amani na Maadili ya kidini Mkoa. Kongamano lilihudhuliwa pia na vikundi tofauti vya kidini toka Wilayani ambao ni wadau waliopokea mualiko wa kuhudhulia ambao ni CCT, TEKI na CPCT. Kongamano liliendeshwa kwa siku mbili.
Lengo la Kongamano hilo lilikiwa ni kuhamasisha amani kwa watu wote bila kujali tofauti zao za kidini ili kuwa na Jamii yenye mshikamano, upendo na Amani kwa watu wote. Mada zilizowasilishwa ni pamoja na Ujenzi wa Maadili na Uzalendo Mada hii iliendeshwa na Askofu ambapo alitoa maana ya Maadili kuwa ni mwenendo mwema ama kutenda haki bila upendeleo kwa watu wote bila kuangalia itikadi zao za kidini au kichama. Aidha Askofu alitoa pia maana ya Uzalendo kua ni hali ya mtu kupenda nchi yake na kua tayari kuitumikia kwa uwaminifu. Ujenzi wa miundombinu ya Amani katika Jamii.
Baba Askofu aliendelea na maada ya pili ya miundombinu ya Amani katika jamaii kwa kusema kua ili amani iendelee kuwepo kwenye jamii zetu ni lazima itengenezewe mazingira ya kuwepo. Alisema Amani ni utulivu wa mazingira mtu anayokaa na Amani ni lazima ihusishe nafsi ya mtu kwa kua chemichemi ya Amani inaanzia ndani ya mtu katika nafsi yake. Aidha aliainisha baadhi ya mazingira ya kutegemea kutengeneza Amani kuwa ni, Makubaliano, Ustahimilivu wa mawazo ya mwingine na Elimu kutolewa kwa jamii.
Mbinu za kutatua Migogogro
Askofu aliendelea kwa kutoa mbinu za kutatua migogoro inapojitokeza katika jamii zetu, alilisisitiza kua watatua hiyo migogoro lazima wawe na utashi wa Kimungu ndani yao kuwawezesha kuona njia sahihi za kutatua migogoro hiyo. Mbinu izo ni, Kutafuta ukweli na chanzo cha jambo hilo pamoja na mbinu sahihi za kutatua, Kushiirkiana na Serikali pale panapohitajika, Kushirikiana na kamati ya Ulinzi na Usalama kutatua jambo.
Aidha Baba Askofu aliainisha njia nyingine ambazo huwa zinatuwa kutatua migogoro kwa kuwa na nafasi ya kusikiza pande zote mbili na kutotumia mbinu zile zile ziliozoshindwa kutatua jambo hilo mwanzoni, akasisitiza kubadiri mbinu ya kutatua jambo lolote litakalojitokeza.
Miundombinu ya kutatua Migogoro ni kama kusikiliza, kuuliza, kuchambua, kushauri (Usihukumu)
Mahusiano ya Dini mbalimbali
Maada hii iliongozwa na Shehe na alianza kwa kutoa maana ya Mahusiano kua ni fungamano, maelewano na masikiliozano kati ya mtu na mtu au kikund cha watu na watu. Aidha alibainisha kua kuna aina mbili za mahusiano;
Mahusiano mema
Mahusiano mema ni kati ya mtu na mtu na jamii na jamii, Aidha Shehe alibainisha kua mahusiano mema haina maana ya kua wanakubaliana kila jambo ila wanakua wanachukulian kila mmoja anaona mawazo ya mwenzake ni ya msingi kama yak wake.
Mahusiano mabaya
Shehe alibainisha kua mahusiano mabaya ni yale yasiyo na msingi wa kuleta Amani bali ni machafuko na migogoro baina wa watu au jamii Fulani Aidha alibainisha mahusiano mabaya sio lazima yatokee kwa dini tofauti, watu wa itikadi tofauti bali yanaweza kua kati ya ndugu na ndugu ama watu wa itikadi moja.
Kamati kuu ya Amani, maadili na uzalendo ya mkoa ilikabidhi maazimio yake kwa mkuu wa wilaya yaliyotokana na mada tajwa zote tatu zilizojadiliwa kwenye kongamano hilo. Lakini pia kamati kuu ya Amani,maadili na uzalendo ya mkoa iliyokuwa inaendesha kongamano hilo ilishauri iundwe kamati ya Amani ya wilaya ikiwa na jumla ya wajumbe 14 yenye kuzingatia idadi sawa toka pande zote mbili yaani 7 waislamu na 7 wakristo.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.