Wilaya ya Ukerewe kupitia Idara ya Elimu imeadhimisha wiki ya elimu ya watu wazima ambapo kilele chake kilikua leo tarehe 03/10/2017 na kufanyika katika shule ya msingi Nakatunguru iliyopo kata ya Nakatunguru. Mgeni rasmi katika maadhimosho hayo alikuwa mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ukerewe Focus Majumbi.
Focus Majumbi amesema kuwa maadhimisho haya sio ya idara ya elimu pekee bali ni ya watu wote na ndio maana maadhimisho hayo yaliambatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali. Amebainisha uwepo wa changamoto ya upungufu wa baadhi ya miundombinu kama vile madarasa, nyumba za waalimu na vyoo kwa baadhi ya shule hivyo kuzitaka jitihada za serikali na Halmashauri, kata na kijiji kuendelea ili kuondoa changamoto hizo. Uwepo wa thana potofu wa elimu bure kuwa wananchi wengi wamekuwa wagumu kuchangia maendeleo ya elimu wilayani tafsiri ambayo sio sahihi. Pia pamekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi kuwalazimisha watoto wao kuto fanya vizuri kwenye mitihani yao na kupelekea kufeli na kuirudisha nyuma ufaulu wa shule, wilaya na mkoa. Hivyo amewataka wazazi wawaache watoto na wawahimize kufanya vizuri kwani elimu ndio msingi wa maisha na ndio urithi mzuri.
Richard Reginard Afisa Elimu msingi amewataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwatengeneza wanafunzi kufikia malengo yao. Pia watawasaidia serikali kutimiza lengo na adhma ya serikali kufikia nchi ya viwanda. Maadhimisho hayo yaliambatana na maonesho na michezo mbalimbali ambayo yaliwaweka pamoja walimu na wanafunzi pamoja na wananchi. Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa pete, mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na magunia na muziki na ngoma.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.