Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla. Leo amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe na kupokea taarifa ya Idara ya Ardhi iliyowasilishwa na Tewe Shabani Afisa Ardhi.
Shabani Ameeleza kuwa idara Ina michoro 13 ya mipango miji, 9 ikiwa ipo kwenye mji wa Nansio na 4 ni Muriti, Murutunguru, Muhula na Bwisya ambapo jumla ya michoro hii inatoa viwanja 7500.
Urasimishaji wa makazi holela Halmashauri imeanza kufanya mikutano na wananchi katika maeneo 8 ambayo ni Bukongo, makazi mapya, kakerege, nakoza, nakatunguru, murutanga, bugorola na kakukuru.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla amewataka kuongeza kasi ya upimaji wa viwanja. Amewataka Halmashauri na idara ishirikiane na ofisi ya Ardhi kanda kuwashughulikia watu wote waliopewa ilani kwa wadaiwa wote na hawajapelekwa kwenye vyombo vya sheria.
Mabulla ameagiza kufikia mwisho wa mwezi huu wote wanaodaiwa na serikali tangu 2018 mashtaka yao yawe yameandaliwa ofisi ya kanda itasaidia watu hawa wanapelekwa kwenye baraza la ardhi.
Mabulla ameeleza kuwa hivi karibuni mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya ataripoti wilayani. Hivyo kazi yake yakwanza ashughulike na watu hawa wanaodaiwa na serikali.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Hellen Rocky amemshukuru Mhe. Mabulla kwa kuwezesha kupatikana kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wilaya wa kudumu kwani hapo awali aliyekuwepo alikua akitokea Mwanza. Amesema Halmashauri itaendelea kushirikiana na idara kutekeleza majukumu yake.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.