Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ndugu Paschal Herman amepokea na kukabidhi jumla ya madawati 374 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe mradi uliotekelezwa kwa kiasi cha shilingi milioni 17.58 fedha za mfuko wa Jimbo zilizotolewa Novemba 20,2024.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Afisa mipango wa Halmashauri hiyo ndugu Daniel Nalingigwa amesema lengo kuu la mradi ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi katika shule za msingi kwa kupunguza uhaba wa madawati uliopo.
".. manufaa ya mradi huu ni kuongeza idadi ya madawati shuleni katika kukabiliana na tatizo la wanafunzi kukaa chini na kwa msongamano mkubwa .."
Nae Kaimu Afisa elimu msingi Bi.Bahati Mwaipasi amesema madawati hayo yamegawiwa kwa shule 18 za msingi kwa kuangalia shule zilizo na uhitaji mkubwa zaidi.
Ndugu Pascal amewataka walimu wote katika shule madawati yanakokwenda kuhakikisha yanatunzwa vizuri ili yadumu na kutumiwa na wanafunzi wengi kwa kipindi kirefu yakiwa na ubora wake.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita imeleta fedha nyingi za miradi kwa ajili ya maboresho katika sekta za afya,elimu,miundo mbinu ya barabara huku akiitaja Ukerewe kuwa miongoni mwa maeneo yaliyonufaika nchini huku akiwataka wananchi kupokea heshima hiyo kwa kubeba umiliki wa miradi hiyo.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndugu Vicent Mbua ametoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita na ofisi ya mbunge kwa kuchochea wananchi kuendelea kuhamasika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya jamii sambamba na kuwataka wakuu wa shule kuweka mkakati wa namna ya kutunza madawati na kufanya marekebisho kwa wakati pale inapobidi.
Robert Chacha ni Mkuu wa shule katika shule ya msingi Ihebo iliyopo kata ya Muriti yeye anatoa shukrani kwa uongozi wa Halmashauri kwani ongezeko la madawati 20 aliyopewa kwa ajili ya shule yake yatapunguza uhaba na kuleta chachu ndani ya jamii yao kuona umuhimu wa kuchangia miradi ya kijamii.
ReplyForward Add reaction |
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.