Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ukerewe kuanzia tarehe 18-19 Februari 2018 ambapo katika ziara hiyo amekagua na amezindua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri kupitia fedha za Serikali.
Majaliwa amefanya kikao na watumishi wa Halmashauri na Serikali na amesema lengo kuu ni kufahamiana na kuwa sehemu yao na watumishi na kuona na kukagua shughuli za maendeleo inayoenda sambamba na kukumbusha wajibu, kutoa msimamo wa Serikali ambao ni kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza kauli mbiu ya awamu ya tano ya “hapa kazi tu”
Majaliwa amekagua na kufungua miradi ya maendeleo kama mradi wa mabweni ya wanafunzi katika shule ya sekondari Pius Msekwa iliyoka kata ya Murutunguru, yaliyogharimu Milioni 259 na kila bweni linauwezo wa kuchukua wanafunzi 160, amepongeza mradi huo wenye viwango na amewataka wanafunzi kutunza miundombinu iliyogharimu serikali ili itumiwe na vizazi vingi vijujavyo.
Akiwakatika shule hiyo Mkuu wa Shule alieleza changamoto ya kuwepo na wanafunzi wengi lakini kukosa gari la shule hivyo Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Mkurugenzi kupeleka gari moja liwe la shule jambo ambalo limepokelewa kwa furaha kubwa na wanafunzi na wakazi wanaozunguka shule hiyo.
Majaliwa amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa, kata ya Igalla Mradi ambao umekua borakwani unahudumia vijiji vingi pia amezindua kituo cha afya cha Nakatunguru na katika kituo hiko amewapa chanjo yam atone kwa watoto wadogo na kupongeza kwa ujenzi wa kituo bora chenye viwango. Lengo la kituo hiko ni kuhakikisha Hospitali ya Wilaya inakuwa hainamsongamano mkubwa ilikuhudumia vizuri wagonjwa wanaotoka katika vituo vya afya.
Jioni Majaliwa amezungumza na Wananchi wengi wa Ukerewe walio jitokeza katika viwanja vya Getrude Mongella ambapo alisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wananchi nyingi zilihusu ardhi, maji na afya. Hivyo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh F. Chang’ah kukutana na watu kila wiki ilikutatua kero za ardhi akiwa pamoja na watumishi wa idara ya ardhi wa Halmashauri.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.