.Ndg. Focus Majumbi Katibu Tawala wa Wilaya ya Ukerewe amewataka wanakamati wa jumuiya za watumia maji kitunza miundombinu ya maji iliyopo katika vijiji ili kuwezesha watu kupata Huduma hiyo. Alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya za Watumia Maji katika Wilaya ya Ukerewe Mkutano uliofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri.
Majumbi amemshukuru Mhe. Rais Dkt John Magufuli kwa kuendelea kuleta miradi ya maji katika Wilaya ya Ukerewe ambapo hali ya upatikanaji wa maji inazidi kuimarika siku hadi siku. "Mradi wa maji Chabilungo unahudumia zaidi ya vijiji 13 hii ni hatua kubwa sana" alisema Majumbi.
Mhandisi William Kahurananga ameeleza kuwa Lengo ni kukutana na wanakamati za jumuiya za watumia katika vijiji ili kuimarisha usimamizi na kujengeana uwezo katika namna Bora ya kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha upatikanaji wa maji unakua endelevu.
Aidha ametoa rai kwa viongozi wa kijiji kuwa na ulinzi shirikishi katika maeneo au vijiji vinavyotekeleza miradi ili kulinda miundombinu ya maji ili iwe ya manufaa kwa vizazi vingi mbele na kuendelea kuwapa wananchi huduma ya maji safi na salama.
Mhandisi Datius Burchard amesisitiza kuwa kila kijiji kuhakikisha wanashirikiana na wanakamati wa jumuiya za watumia maji katika kutunza mazingira pamoja na miundombinu yake.
Aidha kupitia Mkutano huo wanakamati za wanajumuiya za watumia maji wamepata uelewa wa usimamizi wa fedha na ujuzi wa utunzaji wa vitabu vya fedha mada iliyowasilishwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Salvatory Mogesi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.