Mkuu Wa Wilaya Ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe amekutana na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ukerewe Leo Tarehe 22/4/2020 Katika eneo la standi ya zamani lengo likiwa kutoa maelekezo mahususi juu ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.
Magembe Ametoa elimu ya COVID-19 kwa wananchi wa Ukerewe kwa kuwataka Wananchi wazingatie maelekezo na tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya kwani wao Ndio wenye ujuzi na afya ya binadamu.
Aidha ameelekeza kuwa katika kupambana na maradhi Haya imetupasa kuwa na uelekeo wa pamoja kama Wilaya hivyo kupitia hadhara hiyo ameelekeza wanaukerewe kufanya mambo muhimu yafuatayo
Watoto kwenda sokoni na minadani na kuzuruza mitaani sasa MARUFUKU. "Pamekua na watoto wengi ambao wanazurura mitaani bila shughuli maalumu, naelekeza kuwa wakae majumbani na kujisomea" alisema Magembe.
Aidha Watoto kwa kipindi hiki tunapoendelea katika janga hili la maradhi watoto hawataruhusiwa kwenda kanisani au msikitini bali wakae majumbani.
Magembe amesisitiza pawepo na utaratibu wa kuachiana nafasi kwa Waumini wa madhehebu Mbalimbali wanapokua wanashiriki ibada ikiwa ni tahadhari za kulindana na maradhi. "Benchi lililokuwa linakaliwa na watu wanne sasa wakae wawili".
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe amewataka wageni wanaokuja kwa shughuli ya Mazishi wawakilishe Watu wache sana na wote watakaoingia kutoka nje ya Ukerewe wafahamike na waandikwe ili iwerahisi kuwafatilia ikitokea watakua maradhi, hivyo kuanzia sasa baada ya mazishi yoyote yale pasiwepo matanga.
Kuanzia sasa Ibada za Usiku Ni marufuku kwani ufuatiliaji wa tahadhari za corona kama zinafuatwa kwa wakati huo ni ngumu hivyo ibada hizo zisitishwe mara moja.
Maeneo ya starehe kama baa na migahawa ni marufuku kuuza bila utaratibu Wa take away au kwenye meza wakae Wawili tu na sio vinginevyo. Mikusanyiko isiyokuwa Ya Lazima ya Lazima mfano kucheza karata au bao Sasa basi.
Magembe amepiga marufuku Disco kwenye bar au Disco vumbi pamoja na utazamaji wa television vibandani. Kila mmoja atulie nyumbani na sio kuwa na Safari zisizo na lazima.
Wafanya biashara ya boda boda kuacha mara moja tabia ya kukaa kwenye mikusanyiko wakiwa wanasubiri abiria.
Wamiliki wa guests Wazingatie kuchukua taarifa za wateja wao vizuri Ili Kama Kuna Mtu anayetoka mahali ambapo Kuna maambukizi wawekwe karantini.
Magembe amewataka wanaukerewe kujenga tabia na kunawa mikono mara kwa mara ilikujiepusha na maradhi Haya, amewataka kuweka ndoo na sabuni katika kila biashara.
Kwa wauzaji Wa Vitakasa mikono Na ndoo kuuza kwa Bei ambayo sihalali na elekezi ya Serikali hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.