Wilaya ya Ukerewe leo imepokea Mwenge wa Uhuru na kutoka Wilaya ya Ilemela na umekimbizwa katika Wilaya katika kata zaidi ya nane na kuzindua, kuweka mawe ya msingi na ufunguzi wa Miradi mbalimbali za Maendeleo ndani ya Wilaya miradi iliyotekelezwq na Halmashauri, Serikali kuu na nguvu za wananchi.
Miradi yote ina jumla ya zaidi ya bilioni 1.3 na ipo katika hatua mbali mbali za utekelezaji.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2021 Luteni. Josephine Paul Mwambashi amepongeza Wilaya ya Ukerewe kwa jitihada kubwa katika kusimamia miradi ya Maendeleo ambapo miradi yote inaonesha thamani ya fedha.
Miradi hiyo iliyo na manufaa mbalimbali na tija kwa wananchi imeelekezwa kutunzwa na kuhaikikisha inadumu.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa KIkundi cha Bodaboda NYEGEZI NANSIO Ambao haukuweza kuzinduliwa hivyo kuelekezwa kukamilisha hatua iliyotakiwa kukamilishwa kisha kuzunduliwa na viongozi wakitaifa.
Mradi wa Jengo la upasuaji Hospitali ya Wilaya, Mradi wa Mfumo wa GotHOMIS katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe, vyumba vinne vya Madarasa kata ya Nkilizya, jengo Uthibiti Ubora wa Shule, kikundi cha walemavu Tunajitambua Umoja Training Center, Mradi wa maji kijiji cha Nansole, utekelezaji wa Mradi wa Maji kijiji cha Murutunguru, Uzaiishaji wa Machungwa kijiji cha Murutunguru,Ujenzi wa daraja la Mahande, Ukaguzi wa daraja la Kilimabuye kata ya Namagondo.
Aidha katika Mradi wa Daraja la Halwego- Mahande kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Luteni. Josephine Paul Mwambashi ametoa siku kumi na nne kuhakikisha kuwa vibao vya alama kuonyesha kuwa kuna daraja viwekwe, na mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mwanza kuwasilisha viambata vyote vinavyoonesha kuwa alama hizo zimeweka mahali watakapokuwa wamefika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.