Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu (MB) amefanya ziara Wilayani Ukerewe na ametembelea msitu wa Negoma kijiji cha Chankamba ambapo Msitu huo uliokuwa ukitunzwa kwa makubaliano kati ya Halmashauri na TFS umekua na mgogoro pamoja na wananchi wanaoishi ndani ya Msitu huo na kuleta mkanganyiko wa mipaka katika eneo hilo.
Kaya 57 ambazo zinachukua Hekta takribani 27 kati ya hekta 698 za Msitu Mzima.
Kanyasu ameelekeza TFS kwa kushirikiana na Halmashauri wafanye upya upimaji na kubaini mipaka vema na kuhakikisha kaya 57 ambazo awali zilikua zinasomeka ndani ya shamba hilo kutoondolewa bali mipaka hiyo mipya Ndio ipishe kaya hizo na wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida.
Diwani wa kata ya Igalla Bituro Manumbu amepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwani palikua na mkanganyiko mkubwa katika eneo hilo.
Aidha Kanyasu amefika katika fukwe nzuri ya Rubya ambayo inasimamiwa na TFS Rubya ameelekeza TFS wahifadhi wa shamba la miti la Rubya kutengeneza eneo ilo kwani ni moja kati ya fukwe nzuri zaidi katika kisiwa cha Ukerewe. Amemtaka Mhifadhi wa TFS Kanda ya Ziwa kuhakikisha maboresho yanafanywa na eneo hilo linatangazwa.
“Ufukwe huu ni mzuri sana na mchanga wake ni mweupe hivyo TFS ihakikishe eneo hili linakuwa la tija kwa kupaendeleza, kupatangaza na kupaunganisha na watoa huduma za utalii kutoka Mwanza ili kupata wageni na kuongeza uchumi wa nchi”. Alisema Kanyasu.
katika kutembelea vivutio vya vilivyo katika kisiwa cha Ukerewe Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu (MB) amefika na kujionea kivutio cha Halwego Andebezyo eneo lililopo katika kata ya Nduruma. Eneo hilo ni sehemu ambayo ina vilele ambavyo ukisimama juu yake unaweza kuona maeneo mengi yazungukayo kisiwa cha Ukerewe.
Amewataka TFS kuendeleza maeneo hayo kwa kushirikiana na Halmashauri kwani itaongeza pato la Halmashauri.
Bi. Ester Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe ameeleza kuwa Ukerewe ni mahali bora zaidi kuwekeza katika utalii hasa wa fukwe kwani Wilaya inafukwe nyingi na chakula, matunda, maji na huduma zote muhimu kama za afya zinapatikana na watu waukerewe ni wakarimu sana aliongeza Chaula.
Mhe Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kisiwa cha Ukerewe na anawahakikishia kuwa na usalama wao na wageni wote.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu (MB) ametembelea kikundi cha Walemavu wanaojihusisha na ufundi ambao wanatengeneza mizinga ya kisasa ya nyuki kilichopo Kata ya Bukongo.
Kanyasu ametoa rai kwa wanaukerewe kuanza kuzalisha asali kwani ni moja ya chanzo kizuri cha fedha. Na wale wanaofanya shughuli hii basi waongeze thamani ya asali ikiwa ni pamoja na kuwa na vifungashio Bora zaidi, jina kwani wataweza kuvuka mipaka na kuuza hata nje ya nchi, alisema Kanyasu.
“Ni wakati sasa kikundi hiki kinapashwa kiwezeshwe na Halmashauri”. Alisema Kanyasu.
Bi. Esther A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe amesema kuwa Halmashauri inaendelea na utoaji wa mikopo hiyo kwa makundi ya walemavu, wanawake na vijana ambapo katika awamu ijayo kikundi hiko pia kitapatiwa pia mkopo kwa ajili ya kuboresha na kuongezea thamani kazi yao.
Kanyasu ameelekeza TFS Ukerewe pindi wakihitaji kutengeneza Mizinga ya Nyuki wasiache kuwapa kazi hiyo kikundi hiko kwani wanaweza na wanafanya kazi nzuri.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.