Benki ya NMB (PLC) imekabidhi msaada wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya TSH Milioni74, vitu hivyo vimetolewa na Ndugu Abraham Augustino Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa kama sehemu ya kushirikiana na serikali na taasisi zake katika kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe ameishukuru sana NMB benki kwa kuona juhudi za serikali na kuamua kuunga mkono. Amezitaka Shule na zahanati pamoja na hospitali waliopatiwa msaada huo kutumia vitu hivyo vizuri kama mahitaji yalivyo na kuboresha utoaji huduma katika maeneo hayo.
Michango imelenga kwenye sekta mbili ambazo ni Afya na Elimu baada ya kuwa wamepata maombi kutoka katika sekta hizo. Kwa kutambua juhudi za serikali katika sekta hizo katika wilaya ya Ukerewe NMB imeona vema kuunga mkono na kwa hospitali tumetoa Vitanda vya wagonjwa wa kawaida vitano(5) vya wagonjwa wa kawaida na viwili (2) vya uchunguzi pamoja na mashuka 50.
Shule ya msingi Msozi, Shule ya Sekondari Kakerege, Mumbuga, Bukongo, Nakoza, Wamepewa vifaa vya kuezekea madarasa vifaa vyenye thamani ya TSH 5,000,000/-
Nduruma Sekondari Madawati yenye Thamani ya TSH 4,999,000/-
Shule ya msingi Mulezi 4,598,000/-
Chuo cha Ualimu Murutunguru 4,497,500/-,Nansio Sekondari 4,000,000/-Nakatunguru Sekondari 4,981,000/-Irugwa Sekondari 4,999,500/-,Zahanati ya Bwasa vifaa vya kuezekea TSH 4,900,000/-. Na hivyo jumla ya misaada yote ni TSH 74,917,840/-. Alisema Augustino.
Akitoa shukrani Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Bukindo Mhe. Gabriel kalala Gregory amesema Msaada huo utasaidia kusaidia na wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kusomea.
Nae Hellen Rocky Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe amemshukuru Meneja wa NMB Nansio Ndugu Hassan Nyangani kwa kuwa Mdau mzuri wa maendeleo hasa katika sekta za Afya na Elimu na amemtaka kutokuchoka kushirikiana na Halmashauri.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.