Amour Hamad Amour mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa ameongoza mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 ambapo umetembelea miradi sita ya maendeleo katika Wilaya ya Ukerewe na ume kufungua miradi miwili, kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili na kuzindua miradi miwili. Miradi hiyo ya maendeleo inathamani ya shilingi 867,899,185.Kauli mbiu ya Mwenge 2017 ni “shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu”
Amour Hamad Amour kiongozi wa mbio za Mwenge 2017 amewata wananchi wa Ukerewe namna moja wapo ya kukuza uchumi wa nchi yetu kama tukiweka mkazo katika sekta ya viwanda kwa kukuanziasha viwanda na kufufua viwanda na kuvifanya viweze kufanya kazi na kwa namna hiyo itatengeneza ajira nyingi kwa watu na watanzania wote. Itawezesha wananchi kuondokana na utegemezi wa taifa na kuweza kupata mapato kupitia shughuli mbali mbali za za uwekezaji katika viwanda kwa wakezaji wadogo, wakati na wakubwa. Amesisitiza kua kwa kuanzisha viwanda Wilaya ya Ukerewe inaweza kujengeka na kuinuka kiuchumi na kuwa kama miji mingine mikubwa iliyoendelea hapa nchini. Ameyasema hayo alipo kuwa akitoa salamu na ujumbe wa mwenge alipo wasili wilayani Ukerewe.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2017 ni pamoja na ofisi ya Asasi ya Lake Victoria Children (LVC)-Bukongo mradi huo Ujenzi wake umegharimu Tshs. 79,665,000.00 mradi umewekewa jiwe la ufunguzi na kisha Kiongozi wa Mbio za mwenge akagawa vyandarua kwa wazazi wa watoto waliopo hapo kituoni na wanaoishi jirani na kituo. Mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Muriti kwa gharama ya Tshs 425, 925,005.00. Mradi wa uzinduzi wa barabara busangu-mugu-nakamwa-kaseni-nakamwa –kitanga km 17.9 na box culvert kwa gharama ya Tshs 57,139,000.00. Mradi wa ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa shule ya sekondari Busangu mugu kwa gharama ya Tshs. 123,044,400.00 jiwe la ufunguzi liliwekwa. Mradi wa ujenzi wa mradi wa maji Bukindo- Kagunguli Ujenzi umegharimu Tshs 150,150,000.00 jiwe la msingi limewekwa. Mradi wa kiwanda kidogo cha kuchakata muhogo na kutengeneza sabuni kwa gharama ya Tshs 31,975,780.00 na kuwekewa jiwe la uzinduzi.
Ilituweze kupiga hatua kiuchumi wa viwanda wilaya lazima izingatie mambo makuu ambayo ni lazima tuwe na Maeneo ya kuwekeza viwanda, maeneo ya kufanya kilimo ilikupata malighafi zakutosha kuingia katika viwanda mbalimbali, kuweza kuwa na nguvu kazi itakayofanya katika viwanda mbalimbali, kuwa na masoko na kuongeza thamani ya vile tunavyotengeneza na kuchakata viwandani. Ameyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la Uzinduzi katika mradi wa kiwanda kidogo cha kusindika Muhogo na kutengeneza Sabuni-Mukunu.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.