Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Emmanuel Sherembi Leo ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa Madarasa Miradi inayotekelezwa kwa Fedha zilizotolewa na Serikali kupitia mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko19 katika Shule 14 ambayo mpaka sasa yapo yaliyofikia hatua ya boma na mengine kufunga renta.
Sherembi ameelekeza Wasimamizi kuhakikisha madarasa hayo yanayoendelea kujengwa yanajengwa katika ubora wa hali ya juu ili kuwa na thamani Pia yaweze kutumika kwa Muda mrefu zaidi. Wilaya ya Ukerewe inatarajia kukamilisha madarasa jumla 167 kufika desemba 15 mwaka huu ambapo kila darasa litajengwa kwa Tsh. 20,000,000/-.
Aidha amewataka Wakuu wa Shule na walimu wa kuu kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni za manunizi kwa kufanya hivyo miradi itapata vifaa vyenye viwango kama vilivyoelekezwa na wahandisi.
Kadhalika amezitaka kamati za ujenzi za Shule pamoja na Wasimamizi wote kuhakikisha miradi hii ya Fedha zilizotolewa na Serikali kupitia mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko19 inasimamiwa kwa vema na kuhakikisha hakuna mianya ya ubadhilifu wa aina yoyote ili thamani miradi hii iweze kuonekana.
Shule za Sekondari zilizotembelewa leo ni Nakatunguru, Bukanda, Mukituntu, Igalla, Mibungo, Muriti, Busangumugu, Ilangala, Buguza, Cornel Magembe, Bukindo na Bukongo na Shule za Msingi ni Nduruma na Igalla Shule shikizi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.