Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amehudhuria kikao cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa mahesabu, baraza hilo maalumu linaloongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa ngazi ya mkoa na wilaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri.
Abyudi Sanga Mkaguzi wa hesabu mkoa wa Mwanza ameeleza hoja ilizonazo halmashauri kuwa zipo zinazoanzia mwaka wa fedha 2002/2003 hadi mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo jumla ya hoja zilizotolewa ni 239, hoja zilizofungwa ni 67, hoja zilizo katika utekelezaji ni 109, hoja ambazo hazijafungwa ni 63. Ameshauri halmashauri kuongeza juhudi katika kujibu hoja ilikuondokana na kuendelea kupata hati ya mashaka katika ukaguzi wa mahesabu.
Sanga ameeleza kuwa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe italetewa timu ambayo itakuja kufanya ukaguzi maalumu kukagua hesabu. “Timu ya ukaguzi maalumu itaanza kazi kuanzia tarehe 13 mwezi Agosti”. Alisema Sanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amelitaka baraza la madiwani kusimamia kikamilifu halmashauri ili kuepusha kuendelea kutengeneza hoja na kuweka msisitizo na nguvu katika kujibu hoja. Mongella amewataka timu ya menejimenti na wataalamu kujikita katika kujibu hoja na kutoa ushirikiano wa kuweka vielelezo ilikusaudia kuondoa hoja hizo. Pia amemwagiza mkuu wa wilaya kusimamia vema fedha zilizoletwa kujenga kituo cha afya Muriti ambapo serikali imetoa 400,000,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Frank S. Bahati ameeleza kuwa ameunda timu ya wataalamu ambayo inashughulikia na inafuatilia ujibuji wa hoja na hatua mbali mbali zimechukulia na kuongeza mwamko katika kuondoa hoja hizo kuanzia 2002. Pia kumekua na upungufu wa wakuu wa idara, na upungufu wa wahasibu katika ofisi ya fedha.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha amesisitiza kuwa baraza analoliongoza lipo imara na amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Madiwani wataendelea kusimamia kikamilifu halmashauri na wataalamu.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.