Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kwa kupata HATI SAFI katika Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019. Ametoa pongezi hizo katika kikao maalumu cha baraza la madiwani kujadili hoja za ukaguzi kikao kilichofanyika ukumbi mkubwa wa halmashauri kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe George Nyamaha na Katibu ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri Bi Ester Chaula na Kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa Emmanuel Tutuba pamoja na wataalamu wa ofisi yake.
Ester Chaula Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ameliambia baraza la madiwani hali ya hoja zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kufikia mwezi juni 2019 ilikuwa na jumla ya Hoja 93 ambapo kati ya hizo hoja mpya ni 40 na hoja za kipindi cha nyuma ni 53. Utekelezaji wa mapendekezo 93 unaendelea na hadi leo hii mapendekezo 18 yamefanyiwa kazi na hoja zimefungwa na utekelezaji wa mapendekezo 75 yaliyosalia unaendelea. “Katika ukaguzi wa hesabu za serikali mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe imepata HATI SAFI.” Alisema Chaula.
Emmanuel Tutuba Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza amepongeza Halmashauri kwa kufikia mafanikio hayo kwani imekua ni lengo la mkoa kuwa hakuna halmashauri zote ziwe na hati nzuri kwani kupitia kaguzi hizi ni muhimu kwani zinalenga kuhakikisha halmashauri zinakuwa na uadilifu katika matumizi. Pia amewataka wakaguzi wa ndani kufanya wajibu wao ili kusaidia halmashauri kuondokana na hoja za mkaguzi wa nje.
“Nipongeze Baraza lako la madiwani kwa kupata hati safi katika Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ikiwa ni baada ya kupata hati za mashaka kwa miaka mnne mfululizo”. alisema John Mongella.
Aidha Mongella amesisitiza bado kama Halmashauri mnatakiwa kuweka utaratibu wa kujadili hoja za Mkaguzi na kuwasilisha kwa mkaguzi wa nje zikiwa tayari na maoni ya kamati ya fedha pamoja na baraza ili kufunga hoja hizo.
Mongella ameitaka Halmashauri kuongeza uwezo wake wa makusanyo ya ndani na kuhakikisha fedha za asilimia 40 zinazotakiwa kwenda katika maendeleo kwani ni takwa la kisheria. Na serikali katika kuimarisha mapato ilianzisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki (POS) lakini bado kuna changamoto zilizoainishwa na mkaguzi ya wakusanya mapato kutowasilisha benki kiasi cha Tsh milioni 274, hivyo ameelekeza kamanda wa Polisi Wilaya na TAKUKURU atoa siku saba (7) fedha hizo ziwezimewasilishwa benki na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwake baada ya siku saba.
Suala la madeni ya madiwani naelekeza kuwa uhakiki ufanyike kwa kushirikiana na ofisi ya RAS nay awe yamelipwa kufikia tarehe 10 juni 2020, na amesisitiza kumbukumbu zote muhimu za kuthibitisha madeni ya waheshimiwa madiwani zitumike na kukamilisha ulipaji mapema iwezekanavyo.
Mhe. George Nyamaha Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Ukerewe na diwani wa kata ya Kagunguli amewapongeza kwa namna kila diwani alivyoshiriki katika baraza hilo na kwa kuonyesha ukomavu katika kujenga hoja kwa maslahi ya wanaukerewe.
Nyamaha ameeleza namna serikali ya awamu ya tano imewezesha Ukerewe kuwa na hospitali mbili za wilaya, ujenzi wa madaraja mawili moja Bukungu na kilimabuye, fedha wa ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ikiwemo Busangumugu. “ yapo mengi mazuri ambayo Mhe Rais ametekeleza hivyo kwa niaba ya baraza hili natoa shukrani zangu za dhati”.
Aidha amewukuru madiwani wote watendaji wote kwa kufanya kazi vizuri na baraza hilo mpaka kufikia wakati huu, amewatakia heri madiwani wanapojiandaa na mchakato wa kupewa ridhaa katika vyama vyao.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.