Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amehudhuria baraza la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali za mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na hoja za Ukaguzi Maalumu uliofanywa na mkaguzi wa nje. Baraza hilo limefanyika katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe.
Taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) katika Halmashauri ya Ukerewe imeeleza hoja mbalimbali kutokana na ukaguzi huo ambapo Halmashauri inatakiwa kutolea majibu ya hoja hizo.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amepongeza viongozi wa Halmashauri na Wilaya kwa jitihada na ushirikiano unaoendelea kufanyika katika kuiletea Ukerewe. Hata hivyo changamoto hazikosenani kwani kuna hatua zimepigwa lakini kuna baadhi ya maeneo bado yanahitaji msukumo zaidi. “Ni imani yetu tutafika mahali pazuri hivyo tuongeze bidii” alisema Mongella.
Mongella ametoa maelekezo kwa menejiment kukusanya mapato na amewataka madiwani kusimamia matumizi ya Halmashauri. Na ameelekeza kila kikao cha robo hoja za ukaguzi ziwe sehemu ya mjadala kwani kufanya hivyo itapunguza mrundikano wa hoja.
“Kuna baadhi ya halmashauri mkoani Mwanza hazina kiwango kikubwa cha mapato lakini zimewekeza zaidi kwenye ukusanyaji wa mapato kiliko matumizi na zina mpangilio mzuri kitu kinachofanya halmashauri hizo kukua kiuchumi”. Alisema Mongella.
Akizungumzia taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema makosa yaliyopo kwenye taarifa hiyo na majibu yake hayaridhushi. “Siwezi kujiingiza mkenge kwa kuunga mkono majibu hayo” alisitiza Mongella.
Kikao hiko kiliudhuriwa na mwenyeji wa Mkuu wa Wilaya Ukerewe Mhe.Cornel Magembe alisema halmashauri inakabiliwa na changamoto kwenye baadhi ya idara kama idara ya ujenzi na ukusanyaji wa mapato.
Aidha baadhi ya madiwani walitoa malalamiko yaliyopo kwenye kata zao Shida ya upataikanaji wa vitambulisho vya taifa (NIDA) kutokana na kuwepo kwa changamoto ya umbali kwa baadhi ya wananchi wanao tokea mbali kwani kituo kipo Nansio. Alisema diwani wa kata ya Ilangala Mhe George Kalagalira nae Mhe. Dismas diwani wa kata ya Bwisya Alisema wavuvi wamekua waathirika wa tozo nakuongezea. Akijibu matatizo hayo mkuu wa mkoa Mhe John Mongela alisema tatizo la wavuvi linafanyiwa kazi na kuhusu tatizo la vitambulisho vya taifa ni kwa taifa zima.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe. George Nyamaha ameeleza kuwa baraza lake la madiwani limejipanga kusimamia vizuri ili kuhakikisha kuwa wanailetea maendeleo wilaya, aidha ameutaka uongozi wa Mkoa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wilaya ya Ukerewe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Ester A. Chaula amesema kuwa changamoto zote zinaendelea kufanyia kazi na kwa mwaka huu wa fedha ni matumaini yetu kulingana na umakini mkubwa uliowekwa katika matumizi utatufanya kupata hati safi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.