"..Mradi huu utaleta heshima kubwa hapa Ukerewe,ama hakika mmeuthibitishia umma kwamba mnatembea ndani ya maagizo ya Mhe.Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutenga fedha za mapato ya ndani kutelekeza miradi maendeleo.."
Hayo yamesemwa na mkimbiza mwenge kitaifa ndugu Ally Ismail Ussu wakati mwenge wa uhuru ulipoweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa hoteli ya kisasa iliyopo kata ya Nansio.
Akisoma taarifa ya mradi huo Afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ndugu Hashim Kimwaga amesema hoteli hiyo inajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo ambapo hadi kukamilika kwake utatumia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 790,000,000.00 huku akibainisha hali ya utekelezaji hadi sasa kufikia 80% .
Hashim ameongeza kuwa lengo la Halmashauri kujenga hoteli hiyo ni kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri,kutoa huduma bora ya malazi kwa wananchi sambamba na kupendezesha mji wa Nansio.
Ndugu Ussi amewataka wananchi wa Ukerewe kulipa kodi na tozo mbalimbali kwa wakati kwani ndio njia pekee itakayoweza kuwapatia maendeleo kwa kasi huku akiwasihi wananchi hao kuwa wamiliki wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Ukerewe na sio kupinga kila kitu.
Aidha mkimbiza mwenge huyo kitaifa amewasihi wananchi wote kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
Mwenge wa uhuru wilayani Ukerewe umetembelea mradi wa vijana ambao ni wanufaika wa mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri,umezindua bweni katika shule ya sekondari Ukerewe, mradi wa maji, kituo cha afya Kigara na kuweka jiwe la msingi mradi wa hoteli na barabara sambamba na kufungua mradi wa ujenzi wa maduka 42.
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.