Meneja NMB kanda ya Ziwa Ndugu Abraham Agustino amekabidhi vifaa vyenye thamani ya Tsh. 19,600,000/- kwaajili ya kuboresha miundombinu ya elimu wilayani Ukerewe, hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Nansio na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ambapo Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) Focus Majumbi alikuwa Mgeni rasmi aliambatana na Mwenyekiti wa CCM(W) Alli Mambile, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Bi. Hellen Rocky, Walimu wakuu shule za Kweru Mto, Namagondo na Nansio, wanafunzi pamoja na wananchi.
Agustino amekabidhi vifaa vya Ujenzi katika Shule tatu ambazo ni Shule ya Msingi Nansio, na Kweru Mto shule ya sekondari Namagondo, NMB inafanya kazi katika jamii hivyo inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini hivyo uwepo wetu inadhihirisha kuwa ni wadau wa wakubwa wa elimu na sekta ya afya na nyingine kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
Ujio wetu leo katika Shule hii ni sisi kukukabidhi mchango wetu kwa niaba ya jamii ya wanaukerewe ambapo tunakabidhi vifaa vya ujenzi kwaajili ya majengo ya madarasa katika shule tatu(3) na vifaa vyote vya ujenzi vina thamani ya Tsh. 19,600,000. Leo tunakabidhi vifaa katika shule hii ya Msingi Nansio vifaa hivyo ni misumari, mbao,kenchi waya, mabati na saruji vyote vikiwa na thamani ya Tsh.5,000,000/- , Shule ya Msingi Kweru Mto imekabidhiwa misumari, saruji,milango, mbao na misumari vyenye thamani ya Tsh. 9,600,000/- , na shule ya Sekondari Namagondo imekabidhiwa misumari, mbao,kenchi waya, mabati na saruji yenye thamani ya Tsh. 5,000,000/-. Alisema Agustino.
Kwa mwaka 2018 NMB imetenga jumla ya Tsh. 1 Bilioni kwaajili ya hudama ya uchangiaji wa shughuli mbalimbali za kijamii kwa maendeleo ya taifa na mpaka sasa zimeshatumika karibia Tsh 900,000,000/- na katika kanda ya ziwa nimeshatoa misaada zaidi ya shule 50 yenye jumla ya Tsh. 245,000,000/- kwa Ukerewe naamini misaada itaendelea kuja kulingana na maombi yaliyopo na kuidhinishwa na ofisi kuu. Ni matumaini yangu vifaa hivi vitakuwa chachu na kutumika vizuri na hatimaye tuone taaluma inainuka katika shule na wilaya yetu.
Mpaka sasa NMB ina mawakala zaidi ya 35 na wanatoa huduma za benki na kwenye visiwa vya Ukara Gana, Irugwa na Kamasi na ni matarajio yetu kupata mawakala katika visiwa vingine pia ili kuwahudumia wananchi huko walipo bila adha ya kusafiri kuja mpaka kisiwa kikuu Nansio. Tumejiunga na makampuni ya simu karibu yote ili kupata huduma za kibenki na kutokana na kukua kwa tekinolojia kwa mteja kutumia simu popote alipo kupata huduma mpaka kukopa fedha kwa huduma ya NMB KLIKI.
Focus majumbi Katibu Tawala Wilaya ameishukuru kampuni ya NMB kwa msaada mkubwa iliyotoa kwa sekta ya elimu katika wilaya ya ukerewe na amepongeza kwa namna ambavyo imezidi kuwa mstari wa mbele katika kusaidia hasa katika sekta muhimu ya elimu. “Tunashukuru sana kwa mchango wenu katika kuboresha miundombinu ya elimu katika shule zetu tatu ni matarajio yetu kiwango cha elimu kitazidi kukua” alisema Majumbi.
Majumbi amewataka wananchi wa Ukerewe kuchangia maendeleo katika shule katika maeneo yao kwani wanaosoma ni watoto wao lakini pia itaendelea kuwatia moyo wafadhili katika kusaidia maendeleo ya shule hizo kwani mfadhili akikuta jingo limeanza anapata moyo wa kukamilisha hivyo nguvu ya wananchi katika kupunguza changamoto za madarasa katika shule.
George Nyamaha Mwenyekiti wa Halmashauri amewapongeza NMB kwa msaada walioutoa katika taasisi za shule na ameeleza kulingana na jiografia ya Kisiwa cha Irugwa msaada wa NMB kwa shule ya Kweru Mto ni muhimu sana kwani kuna uhitaji mkubwa wa madarasa katika shule hiyo. Aidha amempongeza Meneja wa NMB Nansio Ndugu Hassan Nyagani kwa huduma nzuri na kufanikisha utatuzi na misaada mbalimbali ya kimaendeleo katika wilaya.
Awali katika usomaji wa taarifa za shule zinazokabidhiwa shule ya Sekondari Namagondo inajumla ya wanafunzi 591 ikiwa me ni 336 na ken i 255. Waalimu me ni 16 na ke ni 5 jumla ni 21. Madara jumla ni 12 yanayotumiwa na wanafunzi na uhitaji ni 12.
Shule ya msingi Kweru inajumla ya wanafunzi 907 ambapo me ni 438 na ke ni 469 na shule shikizi kweru mto iliyoanzishwa 14/3/2016 ina wanafunzi 79 ambapo me ni 38 na ke ni 41.
Shule ya Msingi Nansio ina jumla ya wanafunzi 1451 ambapo me 734 na ke ni 717 na ina uhitaji wa madarasa 37 yaliyopo ni 8 na upungufu ni vyumba 29.
Baadhi ya wadau wa Elimu waliohudhuria
Picha ya Pamoja
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.