Katibu tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana amesisitiza watumishi wa Ukerewe kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuondoa hoja zisizokuwa na msingi nyakati za kaguzi za kiserikali.
Ameyasema hayo katika kikao maalum cha baraza la madiwani kwa lengo la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuendelea kusimamia mapato na matumizi ya fedha zote zinazoingia na kuzielekeza mahali husika kulingana na mipango iliyokusudiwa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.