Mhe. Mkuu wa Mkoa John Mongella ameanza ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Ukerewe kuanzia tarehe 16-17 januari 2019 ambapo lengo la ziara hii ya kikazi kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa katika Wilaya ni Ukerewe.
Mongella ameanza ziara yake ya kikazi katika kisiwa cha Ukara ambapo ametembelea na kukagua mradi wa maji Bwisya uliopochini ya kikundi Ukara na kusaidiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri unao gharimu kiasi cha Tsh. 41,000,000/- fedha zilizofadhiliwa na Benki ya NMB. Mkuu wa Mkoa amepongeza juhudi za wananchi hasa wanakikundi wanaofanya kazi nzuri ya kuwasaidia na kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika eneo la Bwisya.
Mhe. Mkuu wa Mkoa John Mongella katika ziara yake katika wilaya ya Ukerewe katika sekta ya elimu ametembelea shule za msingi na sekondari ambapo ametembelea shule ya Sekondari Bwisya ambapo ametoa wito kwa uongozi uweke mazingira rafiki ya kuwezesha wanafunzi kuishi hostel na amewasihi wazazi wanafunzi wasome na wakae hostel ili kuondoa umbali mrefu pindi waendapo darasani, shule ya sekondari Bukiko amewapongeza walimu na wanafunzi amewataka wasome kwa bidii na kuwaasa mabinti kujithamini na kuachwa kudanganywa na kupata mimba.
Mongella ameahidi kutoa saruji mifuko 50, na Mhe. Mkuu wa Wilaya Cornel Magembe ameahidi kutoa mifuko 20 ya saruji, nae Afisa elimu wa Mkoa ameahidi kutoa mifuko 20. Amewasihi wananchi kuendelea kujitokeza ili kuboresha miundombinu ya shule hiyo. Shule zingine zilizo kaguliwa katika ziara ya mkuu wa mkoa ni Mwitongo shule ya msingi, shule ya msingi Kagera, shule ya Sekondari Kakerege ambapo aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara na ameahidi kutoa mifuko 60, mkuu wa wilaya 40 na afisa elimu kumalizia bati zilizokuwa zimesalia katika kuezeka.
Mongella ametembelea Chuo cha Ualimu Murutunguru na ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa majengo mapya katika chuo hiko na amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama chuoni hapo kwani hapo awali maji yalipatikana umbali mrefu.
Sekta ya Afya Mkuu wa Mkoa amekagua na kuridhishwa na ujenzi unaondelea wa kituo cha afya Bwisya, mradi unao gharimu Tsh 860,000.000/- fedha zilizokuwa zimesalia kwenye rambirambi baada ya maafa yam v. Nyerere mwezi Septemba.Msimamizi wa ujenzi kutoka SUMA JKT Luteni Masudi ameeleza kuwa mradi huo unatarajia kuwa umekamilika 17/2/2019.
Mongella ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Muriti ambapo wenye thamani ya Tsh. 400,000,000/= amewataka mainjinia wa halmashauri kuwepo eneo la kazi na kuukamilisha mradi huu kwani upon je ya wakati. “Nataka mradi huu uwe umekamilika kufikia 17 februari 2019, alisema Mongella.”
Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua mradi wa ufugaji wa samaki ziwani ulipo eneo ya kata ya Ngoma, Muluseni amepongeza na amesema ufugaji huo uwe somo kwa wengine kufuga samakikisasa.
Amekagua shamba darasa la kahawa lililopo eneo la ngoma lenye miche 14,000 amewataka idara ya kilimo kuongeza miche zaidi na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo cha kahawa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.