Shirika ya Bima ya maisha la SANLAM kanda ya ziwa limefanya semina ya siku moja kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuhusu huduma ya bima ya maisha inayotolewa na shirika hilo. Shirika hilo lenye makao yake makuu Dar es Salaam Tanzania lililoanzishwa Cape town Afrika Kusini kwa sasa lipo bara la ulaya katika nchi za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Uswiswi, Lebanon, Saudi Arabia, India, Malaysia, Ufilipino, Australia nan chi 34 za bara la Afrika.
Lameck Mazubesi Meneja Masoko SANLAM kanda ya Ziwa akiambatana na maafisa masoko wawili wa shirika hilo ametoa wito kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuweza kujiunga na shirika hilo la bima ilikupata huduma mbalimbali kwa manufaa ya baadae.
Mazubesi ameainisha huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika la bima ya maisha kama vile mafao ya uwekezaji (akiba), mafao ya maisha yatolewayo kwa mrithi, malipo ya mfuko, uwezo wakuchukua akiba kidogo uwapo na dharura, mafao yakusitisha mkataba na uwekaji wa pamoja. Aidha alisisitiza ni vema kwa watumishi kujiunga shirika lao ili kunufaika na malipo watakayoyapata pindi watakapokuwa wamefikwa na matatizo na hivyo kuwa sehemu ya faraja kwao. Faida zingine ni pamoja na kurudishiwa 10% ya michango yako yote kila baada ya miezi 60, kuwa na uwezo wa kuchukua akiba kidogo unapofikwa na dharura, wategemezi kuendelea kulipiwa michango yao hata pale mlipaji anapokuwa amepoteza maisha, msaada kifedha ukipoteza mpendwa wako.
Mazubesi alitoa shuhuda mbalimbali kutoka kwa watu walionufaika na huduma ya shirika hilo la bima ambapo aliainisha kuwa kwa sasa wameingia mkataba na Bank ya NMB na malipo kwa njia ya simu ya mkononi ili kuwarahisishia wateja wao huduma pindi wawapo kwenye matatizo. Alihitimisha kwa kuwataka watumishi kujiunga na shirika hilo la bima ya maisha ili wanufaike na huduma nzuri wanazotoa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.