Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe amezinduazoezi la upuliziaji wa kiuatilifu cha kuua Mbu majumbani linalotekelezwa naSerikali kwa kushirikiana na shirika la Abt Associates chini ya ufadhili waSerikali ya Marekani kupitia USAID na takribani zaidi ya TSH Bilioni 5.015zitatumika katika kufanikisha zoezi hili Katika Wilaya ya Ukerewe.
Zoezi linalotarajiwa kuanza tarehe 3/3/2020 mpaka tarehe 30/3/2020 likiwa na lengo kubwa la kukabiliana naugonjwa wa Malaria ambao kwa mkoa wa Mwanza Wilaya ya Ukerewe Ndio unaoongozakwa takwimu za 2019 ni 39%ya wagonjwa wa nje yani (OPD) walikua na vimelea vyaMalaria na wajawazito 16 kati ya 100 wana vimelea vya malaria.
“Nilengo la serikali kuhakikisha wananchi wake wako na kinga thabiti na Bora ilikuakikisha inakua na jamii yenye afya Bora na kuto kuathiri nguvu kazi ambayoni tija kwa mtu binafsi na nchi”. Alisema Magembe
Magembe ameeleza kuwa zoezi litafanyika katika Wilayayote ya Ukerewe katika kata zote 25, vijiji 76 na vitongoji 514 na kazi hiiitatekelezwa na wananchi wenyewe katika maeneo yao wapatao 1,105 ikiwa ni watu622 wenye mikataba ya muda mfupi na viongozi wa vitongoji hivyo limekua zoeziLenye fursa ya ajira za muda kwa wananchi.
Natoa wito kwa viongozi wote kuanzia ngazi za vitongojimpaka Wilaya kushiriki kikamilifu kwa kihamasisha na kukabiliana na hujuma yaaiana yoyote yenye lengo ovu la kukwamisha zoezi hili lenye tija katika Afya zawanaukerewe. Hatua kali zitachukuliwa kwa atakae bainika kuhujimu utekelezajiwa zoezi hili kwa namna yoyote ile. Aliongeza Magembe.
“Pasiwepo kwa nyumba itakayo achwa katika kunyunyiziakiuatilifu cha kuua Mbu majumbani”. amesisitiza Magembe.
“Ziro Malaria inaanza na Mimi,Ukerewe bila Malariainawezekana”
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.