Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuuunga mkono juhudi za makundi mbalimbali ya wajasiriamali wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi hasa hasa sekta ya uvivu ambayo imebeba shughuli nyingi tegemewa ndani ya Wilaya ya Ukerewe .
“..Mmefanya kitu kizuri kuungana kwa kutambua nguvu ya muunganiko hii itawasaidia kukuza mtaji wenu,itawarahisishia kupata teknolojia kubwa ya uzalishaji na kupata masoko ya uhakika ,Halmashauri haitaacha kuwapatia pesa vikundi ambavyo vitaonyesha uadilifu kwa kufanya kazi na kutoa matokeo chanya..”
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde,Christopher Ngubiagai wakati alipotembelea vikundi vitatu vya Tumaini jema,Wagaiwa na Bukasiga ambavyo vimetengeneza shirikisho la pamoja kwa kifupi TUWABU wanaojishughulisha na shughuli za ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ikiwa ni miongoni mwa vikundi wanufaika wa mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri katika kijiji cha Busangumugu kata ya Namilembe ambapo kwa ujumla walipewa shilingi milioni 351 .
Aidha mbali na shughuli za ufugaji samaki kwa vizimba vikundi hivyo vinajishughulisha na uzalishaji wa barafu za kuhifadhia samaki,mradi wa gari (walilopewa zawadi baada ya kushindanishwa na taasisi nyingine za SADC kupitia mradi wa profit blue) na ununuzi wa samaki ,uvuvi wa dagaa kwa kutumia mtumbwi wa mwendo kasi.
Akisoma taarifa ya shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo Meneja wa kikundi cha Bukasiga Bi.Elizabeth Erasto Majura amesema chama hicho kwa kushirikiana na shirikisho la TUWABU wamepanga kujenga kiwanda cha kukausha dagaa kwa njia ya kisasa kisiwani Gana huku wakimuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuongea na mzabuni waliempatia kazi kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu husika kwa wakati.
“Nawapongeza kwa zawadi ya gari mlilopatiwa na SADC ama hakika mmetuwakilisha vyema.Tutawaunga mkono kwa juhudi zenu njema za kupambana na umaskini kupitia tulichonacho,ziwa letu ni la thamani sana tunaweza kufanya vitu vingi vikubwa cha msingi msikilizane muwe wamoja .”amehitimisha Cde,Ngubiagai
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.