Shule 156 zilizopo katika Wilaya ya Ukerewe zimepatiwa jiko la gesi ikiwa ni sehemu ya motisha kwa walimu ili waweze kupata kifungua kinywa asubuhi na chakula cha mchana. Mkuu wa Mauzo na Masoko Taifa gesi Bw. Domician Mkama amekabidhi majiko hayo ili yakawe chachu kwa walimu kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Mkama amesema Taifa Gas imejipanga kuwahudumia wanaukerewe kwa kuwauzia majiko hayo kwani Nishati safi isiyokua na uchafuzi wa mazingira. Amesema hayo wakati wa makabidhiano ya majiko hayo kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi. Ester Chaula naye kuyakabidhi kwa walimu wakuu na wakuu wa shule zote wilayani hapa na kushuhudiwa na Mgeni rasmi Mhe Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe.
Mkama ameeleza Mtungi mmoja unauzwa kiasi cha Tsh 45,000/- lakini Kwa kuanza utauzwa kwa bei ya Tsh 40,000/- kwa mtungi mdogo
Na walimu watawekewa utaratibu wa kukopeshwa na kulipa taratibu mitungi wa 15 kg. Amewaalika walimu baada ya saa za kazi kuja na kuwa mawakala wa kuuza gesi hizo na kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bi. Ester Chaula Amewashukuru Taifa gas kwa kuwapatia walimu wa gesi hizo kwani Zitakua manufaa kwani itawasaidia kupata chai na ni uhifadhi mzuri wa mazingira.
Amewataka Walimu kutunza vema majiko hayo na yatumike kwa ajili ya walimu wote shuleni na sio nyumbani kwa mwalimu Mkuu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe. Joshua Manumbu Awashukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa walimu katika kazi yao. “Nashukuru sana kwa kufanya hili ukerewe Shule kama taasisi itakua chachu nzuri ya wanafunzi kujifunza kutumia gesi mbadala”. Alisema Manumbu.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe afurahishwa na kampuni hiyo ya kizalendo ambayo imewajali walimu.
“Viongozi wengi wa Wilaya ni walimu na hivyo tunaona changamoto zote za walimu hata katika hili niliona kuwa walimu wanahitaji kupata gas hizi” alisema Magembe.
Aidha Maeneo mengi miti imekatwa na imepungua sana na hivyo mazingira yameharibika. Hivyo ni Wajibu wetu kutumia nishati mbadala wa gesi. “Karibu sana mfanyekazi katika Wilaya yetu ya ukerewe”Aliongeza Magembe.
Afisa Elimu Sekondari Benjamin Sperito ameshukuru sana kwa msaada huo na amewataka kila Shule walimu wapate chai au chakula cha mchana kila siku wakati wa kazi. Kila Shule ulitaweka utaratibu wa kuwa na chakula kwa ajili ya wanafunzi. Shule za Msingi 129 na Shule za Sekondari 27 zote zimepatiwa mtungi mmoja wa gesi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.