Ni muendelezo wa timu ya tathimini na ufuatiliaji kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kutoa maelekezo katika kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja ujenzi wa vibanda 42 awamu ya pili katika soko kuu la Nansio ambapo serikali kuu imetoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 300 kukamilisha ujenzi huo.Ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa na ukamilishaji wa maabara moja katika shule ya sekondari Nakatunguru kwa shilingi milioni 25.
Miradi mingine ni ukamilishaji wa maabara tatu na vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mumbuga iliyopo kata ya Ngoma ambapo serikali kuu imetoa shilingi milioni 105, Shule ya msingi Nantare iliyopo kata ya Ngoma ambapo serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 132.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali, vyumba viwili vya madarasa ya msingi na matundu sita ya vyoo.
Timu hiyo ilihitimisha na miradi ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nampisi, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa,ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo kwa shilingi milioni 52.6 katika shule ya msingi Kilongo kata ya Kagunguli na ukamilishaji wa maabara moja katika shule ya sekondari Lugongo kata ya Murutunguru .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.