Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ukerewe Ndugu George Haule ametoa elimu ya mlipa kodi kwa Timu ya menejimenti na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ikiwa ni sehemu ya kujenga uelewa wa pamoja.
Katika elimu hiyo ndugu Haule ameweka wazi uanzishwaji wa kifungu kipya ndani ya sheria ya Kodi ya ongezeko la thamani(VAT) ambapo Halmashauri itatakiwa kuzuia 3% kutoka kwa wazabuni wa bidhaa na 6% kwa wazabuni wanaotoa huduma mbalimbali .Zuio hili litakatwa kutoka kwenye VAT ya mauzo (output VAT)
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Vincent Augustino Mbua amepongeza juhudi za TRA Ukerewe kwa kuendelea kutoa elimu kwa watumishi na wafanyabiasha huku akiwasihi kutowasahau wazabuni wanaofanya kazi mbalimbali na Halmashauri hiyo.
Sambamba na elimu hiyo ndugu Haule amewaalika wafanyabiasha na wananchi wote wa Ukerewe wenye lengo la kutaka kufahamu zaidi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kufika ofisi za TRA zilizopo kata Nkilizya .
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.