Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ametangaza majina saba ya wajume wa tume itakayo kuwa na kazi ya kuchunguza chanzo cha ajali ya Mv. Nyerere kilichotokea tarehe 20/09/2018 Ukara, Ukerewe. Tume ya uchunguzi imeundwa na itakuwa ikiongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.
Wajumbe wengine watakao kuwepo katika tume hiyo ni Joseph Mkundi Mbunge, Bashiru Hussein Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha maafa, Queen Mlozi UWT, Julius Kalolo Mwanasheria, Kamilius Wambura, Selina Magesa Zamani mtendaji Mkuu TEMESA. Tume hii imepewa muda wa mwezi mmoja.
Aidha Mhe. Rais Ameagiza kuwa Waziri wa uchukuzi aitishe zabuni ya kutengeneza kivuko kikubwa chenye uwezo wa kubeba tani zaidi ya 50 na abiria zaidi ya 200 hivyo taratibu zifuatwe katika kutangaza zabuni ili kuwapa huduma haraka wananchi wa Ukara. Pia kivuko hiko kisimamiwe matengenezo yake ilikuwahudumia wananchi baada ya Mv. Nyerere kuzama.
Awali Mhe. Majaliwa alipokuwa akikagua hatua mbali mbali zinazofanyika katika Kituo cha afya Bwisya, amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na inayofanywa wa timu ya madktari, wauguzi na wengine wote katika kituo hiko, pia ameishukuru Serikali kwa kuwezesha fedha kiasi cha Tsh 400,000,000/- za ujenzi wa kituo kipya kwani kisingekuwepo hali isingekuwa nzuri.
Majaliwa ameagiza zoezi la kugeuza na kutoa Mv. Nyerere majini lifanyike haraka na ametaka miundombinu yoyote itakayohitajika na Jeshi linaloongozwa na Jenerali Venance Mabeyo ipatikane haraka na ianze kazi mara moja.
aidha katika majira ya jioni Waziri wa Uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isackk Kamwelwe Amesema mpaka sasa wamepatikana miili miwili na kufanya jumla ya 226.
amepokea Maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwamba kila mfiwa apate Milion 1 na kila manusura apewe Milion 1 kuanzia kesho tarehe 25/9/2018 asubuhi
Mkuu wa majeshi Nchini Venance Mabeyo kesho apeleke wana jeshi mafundi na wa TEMESA wakakague meli ya temesa iliyopo Mwanza ilikianze kazi ya kubeba wananchi kwa muda. Kivuko kinauwezo wakubeba watu 120.
katika hatua nyingine ya kupoea rambirambi kwa wafiwa umoja wa SHIA umetoa Milioni 7, CCM kupitia Katibu mwenezi bw. Humphrey Polepole, GGM wametoa Milion 30 na wanafanya utaratibu wa kusaidia kuleta Cren ili kuongeza nguvu katika kuheuza kivuko.
Mwananchi kutoka Chibasi ametoa Tsh. 20,000/-
Mhe. Rais amesisitiza Fedha zinazochangwa na walioguswa zitatumika kuwapa rambirambi kwa wafiwa na walionusurika.
Jumla ya michango yote mpaka sasa ni Milion 397,020,000/-.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.