Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amefanya ziara ya siku moja katika kisiwa cha Ukara Wilayani Ukerewe lengo likiwa kukagua maendeleo katika sekta ya afya na elimu.katika ziara hiyo ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Bwisya na shule ya sekondari Nyamanga.
Kituo cha Afya Bwisya ni kituo kinachojengwa kwa fedha zaidi ya milioni 800 ambazo Mhe. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza zijenge majengo hayo baada ya fedha hiyo kubaki baada ya rambirambi kutolewa. Usimamizi wa maelekezo hayo ambapo mpaka sasa ujenzi wa kituo cha afya Bwisya uko vizuri na umefika 95% na asilimia zilizosalia zitakamilishwa ndani ya siku chache zijazo. Alisema Mongella.
Mongella ametoa rai kuwa kasi ya kukamilisha usafi na shughuli zingine za mwisho iongezeke ili wananchi waanze kupatiwa huduma kwa ukamilifu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ametembelea pia Shule ya Sekondari Nyamanga ambayo inajengwa katika kata ya Nyamanga katika eneo ambalo wanafunzi walikua na adha kubwa ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo katika shule za sekondari za Bwisya na Bukiko. Hatua ya ujenzi wa shule hiyo ya Nyamanga ni jambo la faraja ambapo wanafunzi wameanza kusoma katika shule hiyo.
Ukamilishaji wa majengo katika shule hiyo bado unaendelea ambapo maabara na baadhi ya madarasa yapo katika hatua ya kunyanyua boma.
Mongella amewataka watendaji kuongeza kasi katika ujenzi huo kwani shule hiyo ni mkombozi kwa anafunzi waishia Nyamanga na vijiji vya karibu.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameeleza kuwa ujenzi wakivuko kikubwa kitakacho tumika kuvusha watu mizigo na magari kwenda Ukara kinaendelea kuundwa na SONGORO MARINE na kinatarajiwa kuwa kikubwa chenye uwezo wa kubeba gari 20 na abiria zaidi ya 1000.
Ester A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe amesema ujenzi wa kituo cha afya na shule ya sekondari Nyamanga ni muhimu kwani wananchi wa kisiwa cha Ukara watapata huduma bora katika sekta ya elimu na afya. Ameahidi kuhakikisha ukamilishaji utafanyika kwa ubora.
Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe amepongeza na kushukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuiletea Ukerewe maendeleo kwani Serikali inawajali watu wake.
Napenda kukukaribisha Wilaya yetu ya Ukerewe hasa katika kisiwa cha Ukara kuona na kufungua kituo kikubwa cha afya Bwisya ambacho kitakua msaada mkubwa kwa wananchi wote wa tarafa ya Ukara na vijiji vya karibu. Alisema Magembe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.