Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ndugu Gerald G. Mweli (Anaye shughulikia Elimu) Leo amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa katika kata na vijiji mbalimbali na kufurahishwa na miradi hiyo ambayo yote inaonesha thamani halisi ya mradi. Lengo la ziara likiwa ni kutembelea na kukagua miradi ya maenendeleo na kuzungumza na walimu wakuu, wakuu wa shule na maelekezo kuelekea kupokea ajira mpya zaidi ya 5000 watakao pangiwa katika shule mbalimbali nchi.
Mhe Mweli amesema Serikali hii inayoongozwa na Mhe John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko makini kuhakikishisha kuwa walimu wanapatiwa miundombinu wezeshi ili kurahisisha na kutatua changamoto zinazowakabili, ndio maana Serikali inatarajiwa kuajiriwa walimu 5000 ambao kila mwalimu atapangiwa kituo cha kazi moja kwa moja na kati ya walimu hao wapo watakao pangiwa vituo vya kazi katika Wilaya ya Ukerewe.
Tathimini ilifanyika mwaka jana 2020 na ilibainika kuwa kila shule inauhitaji na tulipata takwamu halisi za shule hizo pamoja na za walimu ikiwa ni pamoja na taarifa za mwalimu husika, umri, kituo cha kazi alipo na taarifa zingine. Kupitia mfumo huu wa ajira za waalimu kila mwombaji alikua na nafasi ya kuchagua shule moja kwa moja kulingana na uhalisia na uhitaji wa walimu katika shule ndani ya wilaya husika.
Lengo la kutumia mfumo huu kwa waalimu kuomba kazi ni kuondokana na kabisa na malalamiko ya walimu kuajiriwa na baada ya muda mfupi kutaka kuhama.
Mweli amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu kata kuwapokea vema walimu watakao pangiwa kuja katika Wilaya ya Ukerewe na kuhakikisha wanakuwa wanapata mazingira rafiki ya wao kuendelea kuwepo na kuwa na shauku ya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe amewapongeza waalimu wote kwa ujumla katika wilaya ya Ukerewe kwa juhudi wanazoendelea kufanya katika kunyanyua hali ya elimu kwani ni kwa miaka miwili mfululizo matokeo ya mitihani Wilaya imeshika nafasi ya nne (4) kati ya nane (8) kimkoa.
Magembe amewasihi kuhakikisha kuwa walimu wote watakao pangiwa kujakufanya kazi Ukerewe watakutana na mazingira rafiki ya wao kuishi na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. “ mazingira yetu sio mabaya kama wengi wadhaniavyo bali ni kwasababu tu tupo kisiwani”
Nae Ester A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe na Idara za Elimu Msingi na Sekondari ameahidi kuendelea kushirikiana na walimu wakuu, wakuu wa shule na maafisa elimu kata kuwa walimu wote watakao kuja ukerewe watakua na mazingira mazuri ya wao kufanya kazi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.