Siku ya kifua kikuu duniani inaadhimishwa tarehe 24 ya mwezi Machi, ambapo katika wilaya ya Ukerewe siku hiyo imeadhimishwa kwa watukupatiwa elimu juu ya ugonjwa wa kifua kikuu na dalili zake. Zoezi la kuadhimisha siku hii ya Kifua kikuu duniani hapa wilaya ya Ukerewe imefanyika katika eneo la Selema.
Mratibu wa zoezi hilo la utoaji elimu wa Kifua kikuu ni Dkt. Titus Kaniki amesema maadhimisho haya hufanyika kila mwaka na mwaka huu 2018 yameadhimishwa katika eneo la Selema kata ya Bwiro, ambapo watu wamepewa elimu ya ugonjwa wa kifua kikuu, dalili zake, kujikinga pamoja na matibabu.
Katika maadhimisho hayo watu walipewa ushauri wakidaktari pamoja na kuchukuliwa vipimo bure pasipo na gharama yoyote. Kaniki akiwa ameambatana na wauguzi wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vya afya katika maeneo yao na hospitali ya wilaya na wamesisitiza kuwa matibabu ya kifua kikuu ni bure.
Watuwengi wa Selema na kata ya Bwiro wamejitokeza na wengine kuleta ndugu zao iliwapate matibabu yaliyokua yakitolewa hapohapo. Pia Kaniki ameainisha dalili za kifua kikuu kuwa ni pamoja na kukohoa kwa wiki mbili au zaidi, kukohoa makohozi yenye mchanganyiko wa damu, kutoka jasho kwa wingi hasa wakati wa usiku hata maeneo ya baridi, kupata homa za mara kwa mara wakati wa jioni kwa wiki mbili au zaidi, kupungua uzito.
Ameeleza kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ni ugunjwa wenye uhusiano na ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini ya ukimwi hivyo amewaasa watu kutonyanyapaa wagonjwa kwani wanoumwa ni watu ambao tuponao kwenye jamii.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.