Wilaya ya Ukerewe imepiga marufuku matumizi ya pombe zijulikanazo kama viroba na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika kutekeleza adhma na agizo halali la Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh F. Chang’ah ambaye ni mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa cha kupambana na matumizi na biashara ya pombe aina ya Viroba, na madawa ya kulevya.
Kikosi kazi hiko kimefanya msako na kimefanikiwa kukamata mfanyabiasha mmoja Pius Sanga aliyekutwa na katoni 128 za pombe aina ya kiroba vyenye wastani wa gharama ya shilingi milioni 15.
Msako huo pia umewezesha kukamatwa kwa mtu mmoja anaeitwa Kulwa Deo ambaye amekutwa na misokoto 70 ya bangi na kilo moja (1) unga (madawa ya kulevya). Watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi la polisi na watafikishwa mahakamani.
“Watu kwa kiasi fulani bado wanajihusisha na ulimaji wa bangi katika baadhi ya maeneo nawataka waache mara moja kwani kikosi kazi bado kinaendelea na msako katika maeneo yote ya Wilaya hadi visiwani”, alisema Chang’ah.
Kuendelea kutumia viroba, bangi na dawa za kulevya ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwani vina athari mwilini, pia ni chanzo cha ajali kwani wapo waendeshaji wa vyombo vya usafiri wa barabarani wanatumia hivyo ili kuepukana na matatizo hayo amewataka watu kutokujihusiha kwani ni kinyume na agizo halali la Serikali.
Chang’ah amewataka wananchi kuacha mara moja biashara ya viroba, bangi na dawa za kulevya kwani yeyote atakae kamatwa na kikosi kazi kinachoendelea na msako atachukuliwa hatua kali za kisheria. Ametoa rai kwa wananchi wema kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanao jihusisha na bangi, dawa za kulevya na viroba.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.