Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde Christopher Ngubiagai ameongoza timu ya wataalam kutoka Ukerewe walioshiriki kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kilichofanyika mkoani Mwanza.
Tathimini ya jumla iliyotolewa na mratibu wa mpango wa TASAF mkoa wa Mwanza Bi.Monica Mahundi inasema kuwa kumekuwa na ongezeko la walengwa kupata milo mitatu, ongezeko la watoto wanaokwenda shule na kupata huduma za afya tofauti na ilivyokuwa awali sambamba na ongezeko la miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na shirika la OPEC.
TASAF Ukerewe inaendelea na usimamizi madhubuti katika shughuli za uhawilishaji fedha sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora kwa lengo la kuwanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.