Aliekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ndugu Emmanuel L.Sherembi amewaasa watumishi wa Ukerewe kuendeleza umoja na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha mipango mbalimbali ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Ametoa rai hiyo wakati akikabidhi rasmi ofisi na nyaraka mbalimbali za kiutendaji kwa Mkurugenzi mpya ndugu Vincent Augustino Mbua.
Aidha amewashukuru watumishi wote kwa kazi nzuri kwa kipindi chote walichofanya kazi pamoja.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ndugu Mbua amemshukuru Mhe.Rais Samia kwa kumuamini na kumpa jukumu hilo huku akiahidi kushirikiana na timu aliyoikuta kwa maslahi mapana ya wana Ukerewe na taifa kwa ujumla sambamba na kumpongeza Mkurugenzi aliyekuwepo kwa kazi nzuri ya kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.
".. wananchi wetu wana imani kubwa na sisi watumishi wa umma, tusiiwaangushe,tuwasikilize tutende haki.."
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.