Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya maendeleo ya kimataifa (UKaid) imeingia makubalianao na IMA World Health, kutekeleza mradi wa kupunguza udumavu nchini Tanzania. Asasi kadhaa zilishindana kupata ridhaa ya serikali ya Tanzania na UKaid, kutekeleza mradi husika. Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu mchakato wa kuchagua eneo la mradi na asasi washirika katika utekelezaji wa mradi huu. Mradi huu unatekelezwa katika mikoa mitano ya kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza, geita, Kagera, Shinyanga na Kigoma katika Halmashaurti zake zote kwa miaka mitano yaani 2015-2020. Mradi huu umetenga kiasi cha fedha, shilingi za kitanzania 129,929,000/=, 92,755,000/= kwa utekelezaji hatua ya pili kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.
Mradi huu wa mtoto mwerevu kwa kiingereza ni Addressing Stunting in Tanzania Early (ASTUTE) among children under 5 years of age umetambulishwa na Dkt. Kaniki ambaye ni mmoja wa wawezeshaji walioutambulisha mradi huu kwa Waheshimiwa madiwani ili kuweza kuufahamu na kuwajengea uwezo kuweza kuwawahamasishaji katika maeneo yao ambapo ndio wananchi walipo. Ni vema Ukerewe ikatekeleza mradi huu kama makubaliano yalivyo ili tufungue milango kwa wahisani wengine wa maendeleo. Alisema Dkt. Titus Kaniki.
Tabia lengwa za mradi ni pamoja na mzazi kunyonyesha maziwa ya mama “pekee” kwa kipindi chote cha miezi sita ya mwanzo, mtoto akifikisha umri wa miezi 6 apatiwe chakula mchanganyiko chenye lishe bora ikiwemo samaki, mayai, maziwa, mboga za majani na matunda. Familia kuweka mazingira katika hali ya usafi (kuepuka magonjwa), kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka (kuepuka magonjwa), kwa ukuaji bora wa akili, familia ijenge tabia ya kuongea na kucheza na mtoto. Akina baba, wawapungie kazi wanawake kipindi chote cha ujauzito na unyonyeshaji ili wapate muda wa kunyonyesha, kuwasilisha na kuwatunza watoto.
Mikakati mihsusi ya mradi itakayotumiwa ilikufikia lengo la kupunguza udumavu ni pamoja na kutembelea kaya zote zenye walengwa na kujadiliana kuhusu kuboresha afya na lishe za wajawazito, wanaonyonyesha na watoto wadogo. Kuendesha mafunzo kwa wahudumu wa afya (HFWs) na wale wa afya ya jamii (WAJA) ili waweze kutoa huduma stahiki na kufanya unasihi kwa akina mama kuhusu lishe na afya bora ya mtoto. Kutumia vikundi vya uhamasishaji kuhusu kubadili tabia ambapo maswala mbalimbali ya makuzi na maendeleo mazuri ya watoto yatajadiliwa. Mawasiliano kupitia vyombo vya habari hasa radio, ujumbe kupitia simu za mkononi kufikisha taarifa mbalimbali kwa walengwa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.