Zana haramu za Uvuvi
Idara ya Uvuvi na Mifugo imeendesha zoezi lakukamata zana haramu uvuvi ambapo imefanikiwa kukamata vitu hivyo ambavyo vimekuwa vikitumiwa katika uvuvi ambao umekua ukiharibu mazalia ya samaki na kupelekea kupungua kwa viumbe hao ziwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya ukerewe ametoa rai kwa wananchi wa Ukerewe ambao shughuli yao kuu yakujipatia kipato ni Uvuvi hivyo amewasihi kuachana na uvuvi haramu kwani ni mbaya na endapo watakamatwa watachukuliwa sheria kwa vitendo hivo. Ameyasema hayo alipokua akiongoza zoezi la uteketezaji wa zana hizo haramu kwa mazalia ya samaki na viumbe vyake.
Zana zilizokamatwa na kuteketezwa katika shimo la taka la wilaya Bukongo ni makokoro ya sangara (bs) 5, makokoro vyambo/dagaa (ss) 13, nyavu za timba 173, nyavu za makila macho chini inchi6 zipo 15,kamba za kuvutia kokoro mita 2300. Zana hizi kwa ujumla zina gharimu 75,040,000.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.